Meya wa jiji la Dar es salaam Isya Mwita aliye vaa kofia nyeupe
akicheza Bao na mbunge wa Temeke Mhe. Abdallah Mtolea aliye vaa shati la
maua, katika mchezo huo wa ufunguzi Mchezo ambapo Meya alishinda mchezo
mmoja na miwili wakatoka suluhu
|
Washiriki wa mchezo wa Drafti wakiendelea na mchezo. |
NA
CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI
MSTAHIKI
Meya wa jiji la Dar es salaam Isaya
Mwita amewaomba wadau wamichezo nchini kujitokeza kudhamini mashindano hayo
kwakuwa ni michezo kama ilivyo michezo mingine.
Meya
Mwita aliyasema hayo jiji hapa leo katika uzindua wa mashindano ya mchezo wa
Drafti yaliyofanyika katika viwanja vya mwembe yanga, halmashauri ya Temeke.
Mashindano
hayo ambayo yamedhaminiwa na Meya wa jiji Mwita , yalihudhuriwa pia na Mbunge
wa jimbo la Temeke Abdala Mtolea ,
Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa Drafti ambapo jumla ya washiriki 64
walishiriki.
Meya
Mwita alisema kuwa mchezo huo ni mzuri lakini umekuwa ukizaraulika na kuonekana
kwamba wanaoshiriki mchezo huo niwatu ambao hawana kazi za kufanya.
Alisema
wapo wadau wengi ambao wanatoa vipaumbele kwenye michezo ya mpira wa miguu,
mpira wa pete na michezo mingine huku wakiusahau mchezo huo , jambo ambalo
linaonyesha kuwatenga makundi ambayo wamejikita kwenye mchezo huo.
Alisema
“ Niwaeleze tu kwamba, huu mchezo ni mchezo mzuri kama ilivyo michezo mingine,
leo hii wanaocheza mchezo huu wanazaraulika na kuonekana kwamba niwatu ambao
hawana kazi, wasiojua kujishugulisha, jambo ambalo sio kweli natamani mchezo huu ufahamika kama michezo mingine.
“ Kama
kweli tukiunga mkono mchezo huu, ipo siku tutajenga majina yetu kupitia mchezo
huu kama ilivyokuwa kwenye mpira wa miguu, mpira wa pete, na hata mataifa ya
nje yakatuunga mkono kupitia huu mchezo” aliongeza.
Aidha
Meya Mwita katika hatua nyingine alisema kwamba ataunga mkono chama cha mchezo
huo ili waweze kukisajili na kutambulika rasmi.
Aliongeza
kuwa katika mashindano mengine , baada ya kusajiliwa kwa chama hicho,
yatakutanisha kila halmashauri iliyopo jijini hapa na hivyo kupata mshindi
kutoka kwenye halmshauri husika.
“
Jiji lina halmashauri tano, nataka kwenye mashindano mengine ambayo tayari
chama hiki kitakuwa kimesajiliwa , kila halmashauri itashiriki, na mshindi
atapatikana kutoka kwenye halmashauri nasio mmoja mmoja kama ambavyo tumefanya
leo, ila huu ni mwanzo.
Hata
hivyo Meya Mwita ameahidi katika mashindano yajayo kugharimia nauri na chakula
kwa wachezaji watakao shiriki mashindano hayo na kuwa himzi
wachezaji hao kuuthamini mchezo huo.
Awali
akisoma risala mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Meya wa jiji , Mwenyeiti wa Chama
cha mchezo wa huo mkoa wa Dar es salaam , Kiraba Ngibombi amesema chama kinakabiliwa
na changamo nyingi ikiwemo ukosefu wa ofisi na fedha za kuhudumia na kufanya
usajili wa chama hicho.
Mwenyekiti huyo amemuomba Mstahiki Meya katika mashindano yajayo kuwagharimia
wachezaji chakula na pamoja na nauri kwa ajili ya wachezaji hao.
Post a Comment