Wakina Mama waliohudhuria semina hiyo wakimshangilia Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita alipokuwa akizungumza nao kwenye ufunguzi wa seminahiyo. |
Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na wakina Mama waliohudhuria semina hiyo. |
Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita mwenye kofia katikati akizungumza jambo na Mwanaharakati wa kipindi cha Wanawake Live Joyce Kiri wa kwanza kulia , wakati wa ufunguzi wa semina ya vikundi vya wakina mama vya wanawake Live iliyofanyika Pugu jijini hapa leo.kushoto ni Diwani wa kata ya Pugu Henry Kilewo |
CHRISTINA
MWAGALA,OFISI YA MEYA WAJIJI
MSTAHIKI
Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amesema anatambua mchango mkubwa unaotokana
na wakina Mama na hivyo kuwataka wa kina Baba kuwaunga mkono kwa asilimia 100
katika shuguli za maendeleo.
Meya Mwita alitoa
kauli hiyo jiji hapa jana wakati wa uzinduzi wa Vikundi vya wa kina mama vya
wanawake Live yaliyofanyika Pugu halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
Meya Mwita
alisema wakina mama ndio msingi mkubwa ndani ya familia , Taifa kutokana na mchango ambao huutoa jambo ambalo linaleta ustawi mkubwa maendeleo.
Aliongeza kuwa
licha ya changamoto ambazo hukutana nazo
lakini wamekuwa ni watu wasio kata tamaa
hivyo akasisitiza kuwa wakina baba wanatakiwa kutoa ushirikiano wao kwa silimia
100.
Aidha Meya
Mwita aliwapongeza wa kina mama kutokana na ubunifu waliokuwanao kila kukicha katika
kujitafutia maendeleo na hivyo kuwa msaada mkubwa ndani ya familia zao ikiwemo
kuwasaidia majukumu wakina baba.
“ Natambua
mchango wenu sana, mmekuwa wabunifu , mnajishugulisha kwenye mambo mbalimbali
ya kimaendeleo, mmekuwa mstari wa mbele kutengeneza miradi ambayo inasaidia
kwenye familia zenu bila hata wakina baba kushiriki.
“ Hivi sasa
mmeanzisha vikoba, hii yote ni katika kujituma kwenu ili muondokane na
umasikini, nawapongez sana” alisema Meya Mwita.
Akizunguzungumzia
changamoto zilizopo kwenye dampo, la Pugu Kinyamwezi, Meya Mwita alisema
wameanza kuandaa utaratibu ambao utawasaidia kuondokana na chagamoto hizo.
Alisema
suala la dampo limekuwa ni changamaoto kubwa lakini hadi kufikia Agosti mwaka
huu, uratibu huo utakuwa umeshatolewa.
Akizungumzia
suala la maji , alisema kuwa Kata ya Pugu imekuwa na changamoto hiyo na hivyo
kuwa kero kwa wakina mama lakini kwa sasa upo mpango wa kuwawezesha kupata
visima vitatu vya maji.
Alisema
kwenye shuguli za maendeleo hakuna mambo ya vyama na kwamba viongozi walipo
kwenye nafasi zao wanatakiwa kuwatumikia wananchi wote ili kuhakikisha kwamba
wanapata maendeleo waliyoahidiwa.
“ Kwenye maendeleo hakuna mambo ya vyama, kila
mmoja anahitaji maendeleo, mambo ya vyama hivi sasa tunayaweke kando, ili kupata muda wa kufanya kazi moja tu,
yakuwatumikia wananchi ambao mmetuchagua” alisistiza.
“ Ndani ya
jiji hili tunataka kuleta maendeleo, ili mwaka kesho nikija kusimama hapa yale
ambayo tunayazungumzaleo, tusiyarudie tena na badala yake tuzungumze mambo
mengine.
Post a Comment