Na Masanja Mabula –Pemba .
WAJASIRIAMALI
kisiwani Pemba wametakiwa kuzitambua na kuziendea fursa za kibiashara
ili kufanya biashara yenye tija kwa lengo la kujiletea maendeleo pamoja
na taifa kwa ujumla.
Wito
huo umetolewa na Meneja wa urasimishaji rasilimali na biashara za
wanyonge Tanzania Makame Juma Pandu huko micheweni, Wilaya ya Micheweni
Mkoa wa Kaskazini Pemba.
“Kuzitambua
fursa za kiuchumi na kuziendea na kufahamu changamoto za kibiashara
kutamfanya mfanyabiashara afanye biashara kwa uhakika na ataweza
kujikwamua kiuchumi yeye binafsi na Taifa kwa ujumla” .Amesema meneja
huyo.
Ameongeza
kua baadhi ya wafanyabiashara wanashindwa kutenganisha biashara na
mali zao sambamba na kushindwa kutunza kumbukumbu sahihi za biashara
zao hivyo kupelekea kufilisika kutokana na ufahamu mdogo wa biashara.
Nae
Mkuu wa Idara ya bishara Pemba Ali Suleiman Abeid amewaomba
wafanyabiashara hao kuacha kufanya biashara kimazoea na badala yake
watafute elimu ya biashara ili wafanye biashara itakayowakomboa
kiuchumi.
Kwa
upande wake mratibu wa Mafunzo hayo Zuwena Abdalla Hilali amesema lengo
la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wafanyabiashara wadogo wadogo ili
wafanyebiashara endelevu na yenye tija kwao na taifa.
Ameongeza
pia mafunzo hayo yatawaelimisha wafanyabiashara hao umuhimu wa kutumia
taasisi za fedha ikiwemo mabenki kwa ajili ya kutunza fedha zao badala
ya kutunza fedha majumbani.
Mafunzo
hayo ya siku nne ni muendelezo wa mafunzo yanayotolewa na MKURABITA
kwa wafanyabiashara hapa nchini unahusisha wajasiriamali 50 kutoka
Wilaya ya Micheweni.
Post a Comment