Baada ya JKT Ruvu
kuchezea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Toto Africans ya Mwanza, kocha
msaidizi wa timu hiyo, Azishi Kondo, amesalimu amri na kuongea kwa
unyonge kwamba anasubiri kuona timu mbili zikiungana na timu yake
kushuka daraja msimu huu.
JKT Ruvu baada ya
kichapo hicho, imeshuka daraja ikiwa na pointi 23 huku ikibakiwa na
michezo miwili ambayo hata ikishinda haiwezi kuwaokoa na janga hilo.
Kondo alisema kuwa
japokuwa wameshashuka daraja, lakini hawatakubali kufungwa katika mechi
zao mbili zilizobaki dhidi ya Majimaji na Ndanda FC.
“Sisi tushashuka
daraja na msimu ujao tutacheza Ligi Daraja la Kwanza, kwa sasa
tunasubiri kuona ni timu gani tutaungana nazo, lakini japokuwa
tumeshashuka, hatutakubali kufungwa kwenye mechi zetu mbili zilizobaki.
“Sasa hivi
tunajipanga kucheza na Majimaji katika uwanja wetu wa nyumbani wa
Mkwakwani uliopo Tanga, kisha tunamalizia na Ndanda kule kwao kwenye
Uwanja wa Nangwanda Sijaona na mechi zote tunataka kuibuka na ushindi,”
alisema Kondo.
Post a Comment