SHEREHE
za Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa
kufanyika Mei 24 mwaka huu ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.
Kamati
Maalum iliyoundwa kusimamia tuzo hiyo imefanya mabadiliko kiasi kwa
kuongeza baadhi ya tuzo ambazo hazikuwepo msimu uliopita lengo ikiwa ni
kuboresha tuzo.
Tuzo
zilizoongezwa ni: Tuzo ya Heshima (ambayo itatolewa kwa mwanasoka nguli
wa zamani mwenye historia nzuri kwa soka la Tanzania).
Nyingine
ni: Tuzo ya Kikosi Bora cha Msimu (Itatolewa kwa wachezaji Bora 11 wa
Ligi Kuu (VPL XI 2016/2017) walioteuliwa kutokana na ufanisi wao katika
ligi hiyo msimu huu.
Pia
imeongezwa Tuzo ya Mchezaji Bora mwenye chini ya umri wa miaka 20 (Hii
itatolewa kwa wachezaji waliofanya vizuri katika ligi ya vijana ya timu
za Ligi Kuu ya Vodacom.
Tuzo
hiyo ya Mchezaji Bora wa Ligi ya Vijana itajulikana kama Tuzo ya Ismail
Khalfan ikiwa ni heshima ya kumbukumbu ya mchezaji Ismail Khalfan wa
Mbao FC aliyefia uwanjani katika mashindano hayo yaliyofanyika mkoani
Kagera.
Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) limefikiria kutoa tuzo hiyo kama njia mojawapo
ya kuonesha kuthamini kipaji cha mchezaji huyi wakati wa uhai wake.
Kutokana
na mabadiliko hayo tuzo zitakazotolewa katika sherehe hizo pamoja na
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya VPL ambayo ndiyo tuzo kuu, pia ni
Bingwa wa Ligi Kuu, Mshindi wa Pili, Mshindi wa Tatu, Mshindi wa Nne na
Mfungaji Bora.
Nyingine
ni Mchezaji Bora wa Ligi Kuu, Golikipa Bora, Kocha Bora, Mwamuzi Bora,
Mchezaji Bora wa Heshima, Mchezaji Bia anayechipukia, Goli Bora la
Msimu, Mchezaji Bora wa Kigeni, Mchezaji Bora wa Chini ya Umri wa Miaka
20 na Timu Yenye Nidhamu.
Tuzo za Bingwa, mshindi wa pili, wa tatu na wa nne na Mfungaji Bora hizi zipo kulingana na msimamo wa ligi ulivyo.
Hata
hivyo Mfungaji Bora safari hii kuna wachezaji wawili wamefungana, hivyo
kamati itapitia vigezo vilivyopo katika Kanuni za kumpata Mfungaji Bora
w Ligi Kuu Tanzania Bara ili kupata mshindi ambaye atatangazwa siku
hiyo ukumbini.
Wafuatao wameteuliwa kuwania tuzo hizo kutokana na vigezo mbalimbali:
Mchezaji Bora wa Ligi Kuu
Aishi MANULA – Azam
Simon MSUVA – Yanga
Shiza KICHUYA – Simba
Haruna NIYONZIMA – Yanga
Mohammed HUSSEIN – Simba
(Majina
ya wanaowania tuzo hiyo yalitolewa Jumatano iliyopita na upigaji kura
unaendelea ukiwahusisha Makocha wa timu za Ligi Kuu na Makocha
Wasaidizi,Wahariri wa habari za michezo na Manahodha wa timu za Ligi
Kuu, ambapo mwisho wa kufanya hivyo ni Jumanne Mei 23 mwaka huu).
KIPA BORA
Aishi MANULA – Azam
Owen CHAIMA – Mbeya City
Juma KASEJA – Kagera Sugar
KOCHA BORA
Joseph OMOG – Simba
Mecky MEXIME – Kagera Sugar
Ettiene NDAYIRAGIJE – Mbao
MWAMUZI BORA
Shomari LAWI – Kigoma
Elly SASII – Dar es Salaam
Hance MABENA – Tanga
MCHEZAJI BORA WA KIGENI
Haruna NIYONZIMA – Yanga
Method MWANJALE – Simba
Yusuph NDIKUMANA – Mbao
MCHEZAJI BORA ANAYECHIPUKIA
Mbaraka ABEID – Kagera Sugar
Shaaban IDD – Azam
Mohammed ISSA – Mtibwa
TUZO YA ISMAIL KHALFAN – (U-20)
Shaaban IDD – Azam
Abdalah MASOUD – Azam
Mosses KITAMBI – Simba
TUZO YA HESHIMA
(Atatangazwa aliyeteuliwa siku hiyohiyo ya sherehe za tuzo).
GOLI BORA LA MSIMU
(Tayari yamepatikana mabao bora 10 ambayo yataoneshwa siku hiyo ukumbini ikiwemo lile bora la msimu mzima).
TIMU YENYE NIDHAMU
(Mshindi atatangazwa ukumbini siku hiyo kulingana na vigezo vilivyopo).
WACHEZAJI 11 BORA WA MSIMU – VPL XI 2016/17
(Watatangazwa ukumbini siku hiyo ya sherehe).
Kamati
inayohusika na usimamizi wa tuzo inawaomba wadau wote ambao wameombwa
kupiga kura katika Tuzo ya Mchezaji Bora wafanye hivyo kulingana na fomu
walizotumiwa na mchango wao una thamani kubwa.
Post a Comment