Afisa Vipimo akikagua mawe ya Mizani kabla ya kuanza kuipima
Afisa Vipimo akiandaa mawe ya mizani iliyopitishwa kwa ajili ya kugonga muhuri wa Wakala wa Vipimo
Jiwe la Mizani likiwa limegongwa muhuri wenye nembo ya Bibi na Bwana pamoja na tarakimu mbili za mwaka husika (17)
Stika maalum ikiwa imebandikwa katika mizani baada ya kuhakikiwa na kupasishwa
Afisa Vipimo akikagua rula ya Mizani kabla ya kuanza kupima
Jiwe la Mizani likiwa limegongwa muhuri wenye nembo ya Bibi na Bwana pamoja na tarakimu mbili za mwaka husika (17).
Wakala wa Vipimo nchini imezuia
matumizi ya mizani 94 kati 150 ya vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS)
katika Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, isitumike hadi pale itakapo
fanyiwa marekebisho na kuonekana inafaa kwa matumizi.
Wakala wa Vipimo Mkoani humo
imesema, kuzuiliwa huko kutakwenda hadi msimu ujao wa ununuzi wa ufuta
na korosho, na ili iweze kutumika ni mpaka pale itakapo fanyiwa
marekebisho na Mafundi Mizani na kisha kugongwa mhuri tena kwa ajili ya
matumizi.
Wakala wa vipimo imesema katika
zoezi hilo la ukaguzi wa Mizani Wilayani Ruangwa imehakiki jumla ya
vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) 23 na kukagua jumla ya mizani 150
ambapo kati ya mizani hiyo iliyopimwa na kuhakikiwa kuwa sahihi ni
mizani 56 na iliyozuiliwa kutumika mpaka itakapofanyiwa marekebisho ni
mizani 94.
Kwa mujibu wa wakala wa vipimo
Mizani mingi imeonekana kuwa na mapungufu kama vile kutokuwa na vipimo
sahihi, “Ni kwamba mizani hii tuliyo ipitia tumeabaini ina mapungufu
kuanzia 200g hadi 1kg ambayo kwa kawaida mzani unatakiwa kuwa na
Upungufu unaokubalika wa kiasi cha 80g tu” alisema mmoja ya maafisa wa
wakala wa vipimo.
Ameongeza kuwa, Vilevile baadhi
ya mizani imechakaa na kusababisha kupoteza usahihi katika Upimaji wake
kutokana na namna mizani hiyo inavyo hifadhiwa mara baada ya msimu wa
ununuzi kukamilika, “Mizani mingi huifadhiwa katika maeneo machafu yenye
vumbi ambayo husababisha mizani kupata kutu, lakini pia njia
inayotumika kusafirishia mizani hiyo si salama kwani mizani mingi
husafirishwa kwa Usafiri wa pikipiki mara baada ya msimu mauzo
kukamilika, ambapo husababisha mizani kuangusha baadhi ya vifaa vyake
muhimu wakati wakusafiri”. Imesema taarifa hiyo ya wakala wa vipimo.
Kwa upande wake Meneja wa mkoani
Lindi Bw. Stephen Masawe ameeleza kuwa wameamua kuendesha zoezi hilo la
ukaguzi wa mizani ili kubaini mizani iliyo sahihi na isiyo sahihi ili
kuipitisha kwa ajili ya msimu ujao wa ununuzi wa mazao.”tunaelekea
katika msimu wa ununuzi wa mazao, hivyo kama mkoa lazima tujiridhishe na
mizani iliyopo, kabla msimu haujaanza”, alisema Masawe.
Aidha amesema kwamba, kwa mizani
itakayo hitaji marekebisho mafundi watapita kuifanyia ukarabati kisha
tutaihakiki upya na kama itakuwa sawa basi itapasishwa kwa ajili ya
msimu huu wa ununuzi wa ufuta na korosho.
“Zoezi hili litapunguza sana
gharama za uendeshaji wa vyama vya ushirika vya msingi kwani awali
mafundi mizani walikuwa wanapita na kurekebisha mizani zote, hii ilikuwa
inapelekea nyama vya ushirika vya msingi kutumia gharama kubwa ya
matengenezo hadi Tsh. 400,000= kwa mzani Mmoja lakini kwa sasa mafundi
watapita kurekebisha mizani iliyobainika kuwa na mapungufu ambayo
yameainishwa na Wakaguzi wa mizani tu” alisema Masawe.
Zoezi la uhakiki wa mizani
lilianzia katika Wilaya ya Ruangwa na sasa zoezi hilo limehamishiwa
katika Wilaya ya Nachingwea mkoani humo, zoezi hilo la ukaguzi wa Mizani
ni zoezi endelevu ambalo humsaidia mnunuzi na muuzaji kutopunjana
wakati wa mauzo ya mazao.
Wilaya ambazo hadi hivi sasa
hazijafanyiwa ni Liwale, Kilwa, Lindi Mjini na Lindi Vijijini hata hivyo
wakala wa vipimo amesema zoezi hilo litandelea katika wilaya hizo.
Nao wananchi kwa upande wao
wameipongeza Wakala wa Vipimo kwa kuwapa elimu ya matumizi sahihi ya
Vipimo pamoja na kufanya ukaguzi wa Mizani kabla ya mafundi kupewa tenda
ya kuitengeneza,
Akizungumza kwa niaba ya wnanchi
wenzake ndugu Laurent Adrian Muya, ambae ni mwanakijiji wa Michenga A
amesema, kuhakikiwa kwa mizani kunawapa faraja na inatoa picha kuwa
Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuhakikisha mkulima hapunjwi wala
mnunuzi hapunjiki, “Uhakiki huu wa mizani ni ishara kwamba, Serikali
yetu imedhamiria kumkomboa mwananchi, tunampongeza sana Rais wetu John
Pombe Magufuli, Mungu ambariki”, alisema Laurent.
Kila mwaka Wakala wa Vipimo
huendesha zoezi la Uhakiki kwa nchi nzima inapofikia msimu wa ununuzi wa
mazao ya Biashara na Chakula na katika msimu wa 2017/2018, zoezi hilo
limeanzia katika mikoa ya kusini ya Lindi, Mtwara na pamoja.
Post a Comment