Mwagala
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya
Mwita, akihutubia Umma wa kislamu
uliofika katika dua maalum ya kumuombea
Shekhe Yahya Hussein pamoja na kukaribisha mwezi mtukufu Ramdahani
unaotarajia kuanza mwishoni mwa wiki hii. Dua hiyo ilifanyika katika Makaburi ya Tambaza Jijini Dar es
salaam janaBaadhi ya waumini wa dini ya kiislamu
waliohudhuria dua maalumu ya kuwaombea
marehemu na vipenzi vya Mtume Muhamad (s.a.w) iliyofanyika jana katika makaburi
ya Tambaza, Upanga Mashariki jiji Dar es Salaam
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya
Mwita, akiwa kwenye dua ya pamoja na baadhi ya mashehe waliohudhuria dua
maalumu ya kumuombea Sheikh Yahya Hussein sambamba na kuukaribisha mwezi
mtukufu wa Ramadhani. Dua hiyo ilifanyika jana katika makaburi ya Tambaza
yaliyopo Upanga Mashariki jijini hapa.
Mstahiki Meya Isaya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita mjukuu wa marehemu
Shekhe Yahya Hussein, Yahya Hussein wakati akisoma Quruan Tukufu katika Makaburi ya Tambaza Jijini Dar es
salaam jana
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita,
akipokea risala maalumu iliyoandaliwa na Taasisi ya Shekhe Yahya Hussein katika
dua maalumu ya kumuombea Shekhe Yahya
Hussein pamoja na kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani katika
makaburi ya Tambaza yaliyopo Upanga Mashariki Jijini Dar es salaam jana
Mstahiki
Meya wa jiji la Dar es salaam, Isya
Mwita, akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya mashehe waliohudhuria
dua maalumu ya kumuombea Sheikh
Yahya Hussein sambamba na kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani
katika makaburi ya Tambaza yaliyopo Ukonga Mashariki Jijini Dar es
salaam.
NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI
MSTAHIKI
Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ameahidi kusaidia kupunguza
deni la sh. Milioni 16 linalodaiwa na mkandarasi wa kampuni ya Ushirombo
kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa makaburi ya Tambaza.
Meya
Isaya alisema kuwa kwa nafasi yake atajitahidi ili kuhakikisha kwamba
anasaidia kupunguza deni hilo kama sio kumaliza kabisa kutokana na
umuhimu wawatu ambao wamepumzishwa katika eneo hilo.
Meya
Mwita aliyasema hayo jijini hapa jana wakati wa dua maalumu ya
kumuombea Sheikh Yahya Hussein sambamba na kuukaribisha mwezi mtukufu wa
Ramadhani.
Alisema
kwamba hafanyi jambo hilo kwa ajili ya mambo ya kisiasa ama
kuwafurahisha waisilamu, bali ni kutokana na kutambua umuhimu wa watu
waliolala katika eneo hilo, hasa ukizingatia kila mwanadamu lazima
apitie hatua hiyo.
“
Nimesikia kwenye risala yenu kuwa mnadeni ambalo nikubwa, lakini mimi
sitasema nitachangia kiasi gani, ila nitapunguza kwa nafasi yangu kiasi
ambacho mnadaiwa” alisema Meya Mwita.
“
Watu ambao leo hii tunawakumbuka wamelala hapa, walikuwa na mchango
mkubwa , kila mmoja anatambua hilo, waliweza kuitangaza nchi yetu
kwenye mambo ya dini , lakini pia kwenye mambo mengi ya kimaendeleo ,
hivyo tunatakiwa kutambua na kuwakumbuka” aliongeza.
Aidha
katika hatua nyingine , Meya Mwita aliwasihi waumini wa dini ya
kiisilamu , katika kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuwaeleza
kwamba ni muhimu kuendeleza mambo mema ambayo huyafanya wakati wa mfungo
huo.
Alifafanua
kwamba , imekuwa ni kawaida kwa mwisilamu kutumia kipindi cha mfungo wa
ramadhani kuficha maovu na kutenda mema ,lakini baada ya kumaliza
kipindi hicho huendelea na matendo yasiyompembeza muumba wao.
Alisema
ifike wakati kwa kila muumini ,kutambua umuhimu wa kutenda na
kuendeleza mema ambayo aliyafanya wakati wa mfungo kwani kufanya hivyo
kutamuweka kwenye nafasi nzuri ya kiimani.
“
Kunajambo ambalo ndugu zangu waisilamu huwa mnafanya, wakati wa mwezi
kama huu ambao tunaelekea, kila mwislamu utamuona akihusisha kwenye
mambo mema tu, ale ambao walikuwa hawaswali wataenda msikitini, wale
ambao walikuwa wakitenda mambo machafu ya kumchukiza muumba wao
wataacha”
Lakini
baada ya kipindi hicho cha siku 30 kumalizika kila mmoja atarudi kwenye
tabia yake, sasa hili jambo ni mtihani kwakweli, niwasishi tu, najua
naongea maneno machungu , naninawagusa wengi, tujenge utamaduni
wakuyaendeleza haya badala ya kuacha” alisisitiza Meya Mwita.
Hata
hivyo Mashehe waliohudhuria dua hiyo, walimpongeza Meya Mwita kwakuwa
na moyo wa kujitoa kwenye shuguli za kijamii na hivyo kumuomba kuendelea
na misingi hiyo ili aweze kuwatumikia vizuri wananchi wa jiji
analoliongoza.
Post a Comment