NAIBU INSPEKTA JENERALI WA POLISI,
ABDULRAHMANI KANIKI, AKITOA HOTUBA YA UFUNGUZI WA MKUTANO WA KAMATI
TENDAJI ZA SHIRIKISHO LA WAKUU WA POLISI KWA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA,
(SARPCCO) IKIWA NI MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA SHIRIKISHO
HILO UNAOTARAJIWA KUFANYIKA JUMATANO TAREHE 24/05/2017 MKOANI ARUSHA.
PICHA NA HASSAN MNDEME-JESHI LA POLISI.
BAADHI YA WAJUMBE WA KAMATI TENDAJI ZA
SHIRIKISHO LA WAKUU WA POLISI KWA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA, (SARPCCO)
WAKISIKILIZA HOTUBA YA MGENI RASMI WAKATI WA UFUNGUZI WA MKUTANO WA
KAMATI HIZO IKIWA NI MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA SHIRIKISHO
HILO UNAOTARAJIWA KUFANYIKA JUMATANO TAREHE 24/05/2017 MKOANI ARUSHA.
PICHA NA HASSAN MNDEME-JESHI LA POLISI
Na. Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Arusha.
Mkutano mkuu wa mwaka
wa Shirikisho la wakuu wa Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika
(SARPCCO) unatarajia kufanyika jumatano Mei 24, 2017 mkoani Arusha chini
ya mwenyekiti wa Shirikisho hilo kwa kipindi hiki ambaye ni Mkuu wa
Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu.
Taarifa
iliyotoilewa na Msemaji wa Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Advera
Bulimba imesema mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Waziri wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba na utahudhuruwiwa na
Viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi kutoka SADC na wale wa Shirikisho
la Polisi wa kimataifa INTERPOL ambapo tayari kamati tendaji za
shirikisho hilo zinaendelea na mikutano yake kwa ajili ya maandalizi ya
mkutano huo mkuu.
Bulimba
alisema katika mkutano huo mambo mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo jinsi
ya kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka kwa kufanya Operesheni za
pamoja katika kubaini na kukabiliana na makosa mbalimbali yakiwemo dawa za kulevya, wizi wa magari, usafirishaji haramu wa binadamu na ugaidi.
“Vilevile,
mkutano huu utajadili utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa na Wakuu wa
Upelelezi wa SARPCCO pamoja na kamati tendaji za sheria, Mafunzo na
kamati tendaji ya Jinsia na watoto baada ya mkutano wao uliofanyika
mwezi Machi mjini Bagamoyo” Alisema Bulimba.
SARPCCO
iliundwa mwaka 1995 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa Majeshi ya
Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika katika kukabiliana na vitendo vya
uhalifu. Shirikisho hilo linaundwa na Nchi kumi na tano ambazo ni
Tanzania, Angola, Botswana, Malawi, Lesoto, Mauritius, DRC, Msumbiji,
Namibia, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland, Madagascar na
Syshelis.
Post a Comment