“Kupelekwa nchini Marekani kwa Hassan na washirika wake ni mafanikio yatokanayo na ushirikiano wetu wa muda mrefu na wenzetu katika serikali ya Tanzania katika nyanja nyingi katika sekta za usalama, usimamizi wa sheria na haki. Kesi hii ni mfano mzuri sana wa jinsi tunavyoweza kuimarisha usalama wa kikanda na kimataifa pale tunapofanya kazi pamoja,” alisema Virginia Blaser, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania na katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Mamlaka za Tanzania zilimtia mbaroni Shkuba kwa tuhuma za usafirishaji dawa za kulevya hapo mwaka 2014 baada ya msako wa miaka miwili uliofuatia kukamatwa kwa takriban kilo 210 zadawa za kulevya aina ya heroine huko Lindi Tanzania mwezi Januari 2012. Tarehe 9 Machi 2016,Ofisi ya Udhibiti wa Mali za Kigeni ya Wizara ya Fedha ya Marekani (U.S. Department of theTreasury’s Office of Foreign Assets Control - OFAC) chini ya sheria ya kuwabainisha raia wakigeni walio vinara wa biashara ya dawa za kulevya (Foreign Narcotics Kingpin DesignationAct – Kingpin Act) ilimtaja Hassan na kundi lake kama raia wa kigeni aliye kinara wa biashara hiyo haramu. Kwa taarifa zaidi kuhusu tamko hilo la OFAC, tembelea
HAPA
Mwezi Machi 2016, Jopo la maafisa mashtaka (grand jury) la Huston, Texas, lilipitisha mashtaka
dhidi ya Shkuba na washirika wake kwa tuhuma za kula njama ya kumiliki kwa lengo la kusambaza dawa Za kulevya aina ya heroin nchini Marekani katika kipindi cha kuanzia mwaka 2010 hadi 2015. Hatimaye serikali ya Marekani iliwasilisha ombi rasmi kwa Tanzania la kuwapeleka watuhumiwa hao watatu nchini Marekani.
Post a Comment