Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

Lipumba aikingia kifua RITA, asema hakuna wa kuishitaki mahakamani

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba ameikingia kifua Wakala wa Usajili, Ufilisi, na Udhamini (RITA) kuhusu maamuzi yake ya kusajili wajumbe wapya wa Bodi ya Wadhamini ya chama hicho.

Wakati akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Julai 4,2017 amedai kuwa, RITA ilizingatia vigezo stahiki wakati wa kusajili wajumbe hao kwani wajumbe wa Bodi ya CUF wa awali walimaliza muda wao tangu Agosti 9, 2015 kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.
“RITA ilizingatia vigezo vyote katika kusajili wajumbe wapya wa bodi ya wadhamini, sababu wale walioteuliwa na Baraza Kuu mwaka 2010 walimaliza muda wao wa miaka mitano tangu Agosti 9, 2015,” amesema.
Lipumba amedai kuwa, CUF haikuwa na Bodi ya Wadhamini halali tangu Agosti 2015 hadi Juni 12,2017 baada ya RITA kusajili wajumbe wapya walioteuliwa na Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho.
Amedai kuwa, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad aliyetangaza hivi karibuni kuishitaki RITA mahakamani kutokana na kusajili wajumbe hao kinyume na sheria na katiba ya CUF, hana mamlaka ya kuishitaki wakala huo kwa niaba ya chama hicho.
“Bodi pekee ndio yenye mamlaka ya kufungua kesi mahakamani, sio mimi wala yeye, na hatukuwa na bodi halali tangu mwaka 2015. Bodi halali ilichaguliwa na baraza kuu katika ukumbi wa Shabani Mloo,” amesema.
Labels:

Post a Comment

[facebook]

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget