Taasisi ya TAHMEF (Tanzania Health and
Medical Education Foundation) limetoa huduma bure kwa wananchi wa wilaya
ya Kondoa, Dodoma kupima saratani ya shingo la kizazi.
Zoezi hilo liliendeshwa kwa Muda wa
siku mbili (8-9 Julai 2017) zaidi ya wanawake 500 Wilayani kondoa
walijiandikisha na kupata huduma bure ya elimu na upimaji wa saratani ya
shingo ya kizazi.
Pamoja na kutoa huduma hiyo pia TAHMEF
inaendesha mradi uitwao NURU YA AFYA unaolenga kuwezesha wanawake wasio
na ajira rasmi na kuendelezwa harakati za kumfikia kila mtanzania
kupitia utoaji wa huduma za afya bure kwa wale wenye kipato cha chini
pia kuchangia vifaa na mahitaji mengineyo ya hospitali katika vijiji
mbalimbali, kuongeza uelewa na ufahamu wa watanzania juu ya changamoto
mbalimbali za afya na jinsi ya kukabili changamoto hizo mapema.
TAHMEF ni shirika lisilo la kiserikali
(NGO), lililozinduliwa rasmi tarehe 8 Julai 2016 na Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk. Hamisi
Kigwangalla.
Wanawake wakazi wa Kondoa, Dodoma wakisubiri kupewa huduma ya upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi.
Post a Comment