Baadhi
ya wananchi wa Pwani na Dar es Salaam wakiwa ofisi za Wizara ya ardhi
mida ya saa 9 usiku kusubiri kusikilizwa kero zao za ardhi na Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi akitatua
kero za ardhi za wananchi wa Pwani na Dar es Salaam waliofika ofisini
kwake.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi akitatua
kero za ardhi za wananchi wa Pwani na Dar es Salaam waliofika ofisini
kwake.
Mkazi wa Goba jijini Dar es salaam Bibi Fatuma Shami akipata ufafanuzi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi kuhusu eneo lake kuvamiwa na kupata miliki pandikizi.
Mkazi wa Kibaha Mkoa wa Pwani Bibi Mariam Hamis akipata ufafanuzi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi kuhusu eneo lake lililo na Mgogoro.
Baadhi
ya wananchi kutoka Wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani wakimueleza Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi kuhusu
mgogoro wao wa ardhi katika ofisi za Wizara ya ardhi.
Watumishi
wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa Kanda ya Dare s
salaam na Pwani waliokesha na Waziri Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi wakati wa kutatua migogoro ya
ardhi kutoka kwa wananchi.
…………………………………………………………
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ajikuta akikesha ofisini kwake
pamoja na wananchi takriban 189 wenye Matatizo na Kero za ardhi.
Mhe. Waziri ametumia takriban saa
20 kusikiliza kero za wananchi ambao waligoma kuondoka ofisini kwake
hadi kero zao zitakapopatiwa ufumbuzi. Kazi hiyo ilianza majira ya saa 2
asubuhi hadi saa 9 usiku.
Hata hivyo wananchi walilazimika kulala Wizarani wakisubiri kuonana na Waziri kutokana na uwepo wa idadi kubwa ya wananchi hao.
Wananachi wengi wenye matatizo na
Kero za ardhi kutoka maeneo ya Bagamoyo, Kibaha, Mkuranga, Kibiti na
Dar es salaam kwa ujumla wametumia fursa hii ya kipekee ya kuonana na
Waziri mwenye dhamana ya Ardhi na kumuelezea kero zao na hatimaye
kupatiwa ufumbuzi papo hapo.
Wananchi hao wamesifu hatua hii
ya Waziri Lukuvi kukutana nao ana kwa ana na kuzitatua kero zao za ardhi
kwa kuwa haijawahi kutokea. Nae Bwana Francis Kamara mkazi wa Ilala
jijini Dar es salaam amemuomba Waziri aweze kuwaajibisha watumishi ambao
wanakwamisha jitihada zake hadi kupelekea yeye kukutana na wananchi
moja kwa moja.
Mwanzoni mwa mwezi Juni 2017
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi
alitoa Tangazo la kuwataka wakazi wa kanda ya Dar es Salaam na Pwani
ambao wangependa kumuona, wafike katika ofisi yake ya kanda ya Dar es
Salaam iliyopo ghorofa ya pili, jengo la Wizara ya Ardhi – Magogoni,
Kivukoni ili kujiandikisha majina yao, anuani na namba zao za simu.
Aidha, Mhe. Waziri atafanya ziara
kama hii katika kanda nyingine mara baada ya kukamilisha zoezi hilo
katika Kanda ya Dar es Salaam na Pwani.
Post a Comment