Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipata chakula na manahodha na
mabaharia wa meli ya MV Liemba inayofanya safari katika Ziwa Tanganyika.
Muonekano wa meli kongwe ya MV.
Liemba ikiwa imetia nanga katika bandari ya Kigoma, meli hiyo imeatkiwa
kuongeza safari zake kutoka awamu tatu hadi kumi kwa mwezi.
…………………………………………………………………..
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, amewataka manahodha na mabaharia wa
meli ya MV. Liemba kufanyakazi kwa ubunifu na uadilifu ili kuiwezesha
meli hiyo kujiendesha kibiashara.
Akizungumza na wafanyakazi wa
meli hiyo Prof. Mbarawa, ameelezea kuridhishwa na mabadiliko
yanayoendelea katika meli hiyo na kuwataka wasibweteke bali waongeze
ubunifu.
“Hakikisheni mnatoa huduma bora
kwa wateja wenu na kupata faida ili serikali na wadau wengine wawaamini
na kutumia huduma yenu”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Waziri Prof. Mbarawa ameitaka
meli hiyo kuongeza safari zake kutoka awamu tatu hadi kumi kwa mwezi ili
kuhuisha huduma za usafiri na uchukuzi katika Ziwa Tanganyika.
Prof. Mbarawa ambaye yuko katika
ziara ya ukaguzi wa miundombinu mkoani Kigoma amepata fursa ya kukagua
utendaji wa meli ya MV. Liemba, kupata chakula cha pamoja na wafanyakazi
wake katika meli hiyo na hatimae kutoa maelekezo kwa manahodha na
mabaharia wa meli hiyo kongwe hapa nchini.
Post a Comment