Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimfafanulia jambo Mkuu wa Mkoa wa Tanga,
Martine Shigela (kulia) kabla ya kiongozi huyo kuanza ziara yake mkoani
humo. Katika mazungumzo yao ambayo yalifanyika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa
huyo, Masauni aliwataka maafisa uhamiaji pamoja na Polisi kuongeza kasi
ya kutafuta mizizi ya wahamiaji haramu mkoani humo. Kushoto ni Kamanda
wa Polisi Mkoa huo, Benedict Wakulyamba. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kushoto) akimsikiliza Mkuu wa
Mkoa wa Tanga, Martine Shigela (katikati) alipokua anatoa taarifa ya
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo, kabla ya kiongozi huyo kuanza
ziara yake mkoani humo. Katika mazungumzo yao, Masauni aliwataka Maafisa
Uhamiaji pamoja na Polisi kuongeza kasi ya kutafuta mizizi ya wahamiaji
haramu mkoani humo. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Benedict
Wakuliamba. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akitoka kulikagua jengo la Ofisi
ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tanga ambalo linahitaji matengenezo ili
kulirudisha katika hali yake ya kawaida. Hata hivyo, Masauni alimuagiza
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba (kulia)
kuhakikisha jengo hilo linatengenezwa haraka iwezekavyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimfafanulia jambo Mkuu wa
Mkoa wa Tanga, Martine Shigela (katikati) na Katibu Tawala wa Mkoa huo,
Zena Saidi, kabla ya kiongozi huyo kuanza ziara yake mkoani humo. Katika
mazungumzo yao ambayo yalifanyika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huyo,
Masauni aliwataka maafisa uhamiaji pamoja na Polisi kuongeza kasi ya
kutafuta mizizi ya wahamiaji haramu mkoani humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akizungumza na Viongozi wa Taasisi
zilizopo chini ya Wizara yake, mkoani Tanga wakati kiongozi huyo
alipofanya ziara yake kikazi mkoani humo. Katika mazungumzo yao, Masauni
aliwahasa viongozi hao kuhakikisha wanafanya kazi kwa kujituma zaidi na
kuwahakikishia kero zote walizompa atahakikisha anazifanyia kazi.
Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Benedict Wakulyamba.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Post a Comment