Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Mhe. William Lukuvi awasili mkoani Tanga kutatua migogoro ya
ardhi inayoukabili mkoa huo pamoja na mikoa inayopakana nayo.
Katika ziara hii Waziri Lukuvi leo
amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela na Mkuu wa Mkoa
wa Manyara Mhe. Joel Bendera ili kutatua migogoro ya mipaka iliopo kati
ya Wilaya ya Kiteto Iliyopo Mkoani Manyara na Wilaya ya Kilindi iliyopo
mkoani Tanga ikiwa muendeleo zo wa mikutano ya kuutafutia ufumbuzi
mgogoro huu ambao umesababisha uvunjifu wa amani.
Waziri Lukuvi anatekeleza agizo la
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambae alimuagiza Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kutatua mgogoro huu
uliodumu kwa miaka mingi kati ya Wilaya hizo mbili pindi alipofanya
ziara yake mkoani Tanga.
Ikumbukwe mnamo tarehe 18 Januari, 2017
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifanya ziara Wilayani Kilindi katika
Kijiji cha Mafisa na kuzungumza na wanachi Kijijini hapo kuhusiana na
mgogoro huo na kutoa maagizo kwa viongozi wa kuchaguliwa kuacha kutumia
nafasi zao vibaya kuongoza kwa mihemko au ushabiki kwa kuwa kufanya
hivyo kunapelekea wananchi kufuata ushabiki na
kuvunja sheria zilizopo.
kuvunja sheria zilizopo.
Ili kutekeleza agizo hili wakuu wa
mikoa hii miwili wakiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Mhe. William Lukuvi wamekutana ikiwa ni muendelezo wa vikao vya
kulitafutia ufumbuzi suala hili.
Aidha, wawakilishi wa wakazi wa kata ya
Mnazi wilayani Lushoto na viongozi wa Halmashauri ya Lushoto
walimlalamikia Waziri Lukuvi kuhusu mashamba matatu ya Mnazi
yaliyotelekezwa na mmiliki wa mashamba hayo ajulikanae kwa jina la
Le-Mash Enterprises Limited.
Baada ya Waziri Lukuvi kusikiliza
malalamiko hayo, ameahidi kutembelea mashamba hayo kesho ili kujionea
hali halisi na kuwasikiliza wananchi ambao wanakabiliwa na mgogoro huu
ambao umekuwepo kwa miaka mingi.
Post a Comment