Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Sania Suluhu Hassan akihutubia mara baada ya
kukabidhiwa ulezi wa chama cha Girl Guides Tanzania kwenye ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa
Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Sania Suluhu Hassan akikabidhiwa bendera kama
ishara ya kukubali ulezi wa chama cha Girl Guides Tanzania kutoka kwa
Mlezi aliyemaliza muda wake Mama Salama Kikwete ambaye amekuwa mlezi wa
taasisi hiyo hapa nchini kwa miaka 12, hafla hiyo ya makabidhiano
ilifanyikakwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Baadhi ya wanafunzi wakiimba shairi.
………………………………………………………………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewahimiza wazazi na
walezi nchini kuwalea vijana wao katika maadili mema ili waje kuwa
viongozi au raia wema ambao watakaoliletea taifa tija na sifa ya uongozi
bora ndani na nje ya nchi.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu
Hassan ametoa maelekezo hayo katika hafla ya kukabidhiwa kuwa mlezi wa
Tanzania Girl Guides Association (TGGA) kutoka kwa mlezi anayemaliza
muda wake Mama Salma Kikwete katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa
Jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu
Hassan amesema ili kazi ya kujenga maadili mema iweze kufanyika vizuri
nchini ni muhimu kwa wananchi wote kuunga mkono jitihada zinafanywa na
Serikali kwa sasa za kupambana na watu wanaovuruga maadili ya Kitanzania
ili tabia hiyo iweze kukomeshwa haraka.
Amesema kuwa Serikali imejipanga
ili kuhakikisha rasilimali zinazopatikana nchini zinanufaisha wananchi
wote wakiwemo vijana wa kike na wa kiume.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu
Hassan amekipongeza Chama cha Tanzania Girl Guides Association kwa
jitihada zake za kueneza misingi na stadi za kuishi kwa
uadilifu,uzalendo kwani kufanya hivyo wanajenga taifa lenye watu
waadilifu.
Makamu wa Rais pia ameuhakikishia
uongozi wa chama hicho kuwa atakuwa nao bega kwa bega katika
kuhakikisha chama hicho kinajiendesha kwa faida bila kutegemea wafadhili
ambao wanazidi kupungua kila uchao.
“Niwaombeni mbuni mpya za
kujiongezea kipato ili kuwaongezee uwezo wa kujiendesha mbinu hizo ni
kama kutumia ardhi mliyonayo kwa kukopa benki au kuingia ubia na
makampuni yaliyo tayari kushirikiana nanyi ili muweze kujenga majengo
yenu ambayo mtaweza kupangisha na kupata kodi ambazo mtaweza
kujiendesha, kujiongezea kipato na kuendesha chama kwa tija na ufanisi
zaidi”. Amesisitiza Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake, Mlezi wa Chama
cha Tanzania Girl Guides Association aliyemaliza muda wake Mama Salma
Kikwete amesema katika kipindi cha uongozi wake chama hicho kimeweza
kuongeza idadi ya wanachama kutoka 97,000/=mwaka 2015 hadi zaidi ya
wanachama 100,000 kwa sasa na jitihada hizo bado zinaendelea.
Amesema anaimani kuwa chini ya
Uongozi wa Mlezi mpya Mhe Samia Suluhu Hassan Chama hicho kitafanya kazi
vizuri zaidi katika kuwalea vijana wa kike katika maadili mema ili
waweze kujiepusha na vitendo vibaya katika jamii ikiwemo matumizi ya
dawa za kulevya.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ikulu- Dar es Salaam
12-Julai-2017.
Post a Comment