Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (kulia) akifurahia jambo na
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Phillip Mpango (kushoto) na Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Susan
Kolimba na Katibu Mkuu sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho (mwenye
mkoba mweusi) leo walipokutana kwenye Jengo la Watu Mashuhuri la
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha
Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (TBII-JNIA), Bw. Joseph Nyahende
(wa pili kushoto) akitoa ufafanuzi wa namna abiria wenye viza
wanavyohudumiwa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe.
Prof. Makame Mbarawa (mwenye miwani kifuani). Pembeni ya Waziri ni
Katibu Mkuu sekta ya Uchukuzi, Dr. Leonard Chamuriho na nyuma mwenye
suti nyeusi ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania, Bw. Salim Msangi
Mkuu wa Kitengo cha Idara ya
Uhamiaji Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Bw.
Flugence Andrew (kulia) akitoa maelezo ya utaratibu unaotumika kulipia
viza kwa Mhe. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
leo alipofanya ziara kwenye jengo la abiria la kiwanja hicho.
Afisa
Forodha Msaidizi, Bw. Hezron Giso (kulia), akielezea shughuli
anazozifanya ndani ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(TBII-JNIA), kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof.
Makame Mbarawa (mwenye miwani kifuani), wakati wa ziara ya Waziri
iliyofanyika leo.
Afisa
wa Benki ya NMB, Bi. Leah Rutayungurwa (aliyendani ya dirisha) leo
akimmsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof
Makame Mbarawa aliyetaka kujua muda anaohudumiwa abiria mmoja wakati
akilipia viza kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(TBII-JNIA).
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa leo akiwa
katika mfumo wa kupokelea mizigo kwa abiria wanaowasili kwenye Kiwanja
cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere alipofanya ziara ya
kutembelea maeneo mbalimbali. Mwenye kizibao ni Kaimu Mkurugenzi wa
kiwanja hicho, Bw. Joseph Nyahende.
Katibu
Mkuu wa chama cha madereva wa taxi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa
cha Julius Nyerere, Bw. Simon Mwampashi (kulia), akitoa maoni mbalimbali
kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame
Mbarawa leo alipofanya ziara JNIA.
Mhe.
Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha
Julius Nyerere (TBII-JNIA), mwenye kizibao akielezea jambo katika meza
ya ukaguzi wa tiketi za abiria wanaosafiri. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi.
Post a Comment