Muonekano
wa daraja la waenda kwa miguu lililopo eneo la Furahisha, mkoani
Mwanza. Ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99 na limejengwa na kampuni
ya Nyanza Roads Works.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), na
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongela (kulia), wakishuka ngazi za
daraja la waenda kwa miguu lililojengwa eneo la Furahisha, alipokagua
ujenzi wake mkoani Mwanza.
Mhandisi
Mkazi anayesimamia uboreshaji wa kiwanja cha ndege cha Mwanza Bw.
Geofrey Asulumenye, akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, upanuzi wa njia za kurukia ndege
katika kiwanja hicho mkoani humo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili
kulia), akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mkazi Bw. Geofrey Asulumenye
(kulia), kuhusu uboreshaji wa kiwanja cha ndege cha Mwanza, alipokuwa
akikagua uwanja huo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema ujenzi
wa Daraja la waenda kwa miguu lililopo eneo la Furahisha na barabara ya
kutoka Furahisha hadi Pasiansi yenye urefu wa KM 2.7, imekamilka kwa
asilimia 99 Mkoani Mwanza.
Prof.
Mbarawa amesema hayo wakati alipokuwa akikagua maendeleo ya ujezi wa
daraja hilo katika ziara yake ya kikazi mkoani humo na kuridhishwa na
ukamilishwaji wa ujenzi wake.
“Daraja
hili litaondoa changamoto kwa wananchi wanaotembea kwa miguu na
litapunguza au kuondoa adha ya msongamano wanaovuka kutoka upande mmoja
kwenda upande mwingine”, amesema Prof. Mbarawa.
Prof.
Mbarawa amewataka wananchi kutunza daraja hilo na miundombinu yake ili
liweze kutumika kwa muda mrefu kwani limekuwa nembo ya Mkoa wa Mwanza.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongela, ameishukuru Serikali kupitia
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kujenga Daraja la
Furahisha kwa kuwa limebadilisha mandhari ya Jiji hilo.
“Jiji
la Mwanza ni kitovu cha Kanda ya Ziwa, wananchi wameguswa moja kwa moja
na mradi wa ujenzi wa daraja hili”, amesema Bw. Mongela.
Kwa
upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa
Mwanza, Eng. Marwa Rubirya amemweleza Prof. Mbarawa kuwa kazi iliyobaki
katika daraja hilo nikuweka taa za urembo.
Ameongeza
kuwa Daraja hilo pamoja na barabara yake zimegharimu kiasi cha zaidi ya
cha shilingi Bilioni nne na linatarajiwa kuanza kutumika ndani ya siku
mbili zijazo.
Katika
hatua nyingine, Prof. Mbarawa amekagua upanuzi wa barabara ya Makongoro
hadi Uwanja wa Ndege wenye urefu wa KM 5.3, ambapo malipo ya awali
yameshalipwa kwa mkandarasi na mradi unatarajiwa kukamilika mapema kabla
ya muda ambao umepangwa mwezi Mei mwakani.
Prof.
Mbarawa amekagua uboreshaji wa kiwanja cha ndege cha Mwanza ambao
umehusisha ujenzi wa jengo la mizigo, barabara za njia za ndege, jengo
maalum la kuongozea ndege (Control Tower)
na upanuzi wa urefu wa uwanja hadi kufikia KM 3.8 na kuagiza TANROADS
kusimamia uboreshaji wa kiwanja hicho ili kikamilike kwa wakati
uliopangwa.
Amesema
kuwa hatua inayofuata ni kujenga jengo la kisasa la abiria lenye hadhi
ya kimataifa ambalo litachukua na hadhi ya kiwanja hicho.
Uboreshaji
wa viwanja vya ndege nchini ni moja ya mkakati wa Serikali katika
kukuza sekta ya usafiri wa anga na kuongeza pato la Taifa.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Post a Comment