Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano -
Sekta ya Mawasiliano, Injinia Angelina Madete amesema uanzishaji wa
Taasisi ya Teknolojia ya Ufundi (ICoT), utasaidia kupunguza pengo
lililopo sasa baina ya wahandisi, mafundi sanifu na mafundi mchundo
hapa nchini.
Akifungua warsha
ya wataalam washauri na wadau wa Taasisi ya Teknolojia ya Ufundi Jijini
Dar es salaam leo, Mhandisi Madete amewataka wataalam hao kufanya
uchambuzi wa kina ili kuwezesha taasisi hiyo mpya kukidhi mahitaji ya
mafundi sanifu na mchundo na hivyo kukidhi uwiano wa kimataifa unaotaka
mhandisi mmoja, fundi sanifu watano na mafundi mchundo 25.
“Tunataka
kuwa nchi ya viwanda vya kati ifikapo mwaka 2025, hivyo ni lazima tuwe
na wahandisi, mafundi sanifu na mafundi mchundo wa kutosha
watakaofanyakazi kwa weledi na kumudu ushindani katika soko la ajira”,
amebainisha Injinia Madete.
Mhandisi
Madete amesema kuwa pengo la wahandisi, mafundi sanifu na mafundi
mchundo limeongezeka kutokana na vyuo vingi vya kati kutoa shahada hivyo
uwepo wa ICoT utakabiliana na kumaliza changamoto hiyo.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano – Sekta ya
Mawasiliano Mhandisi Angelina Madete akisisitiza jambo alipokuwa
akifungua warsha kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi
(ICoT) jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya ECOM Research Group Ltd, Profesa Godwin Daniel Mjema
akifafanua jambo mbele ya wadau wa sekta ya ujenzi wakati wa warsha
kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) jijini Dar
es Salaam leo.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya ECOM Research Group Ltd, Profesa Godwin Daniel Mjema
akifafanua jambo mbele ya wadau wa sekta ya ujenzi wakati wa warsha
kuhusu uanzishwaji wa Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (ICoT) jijini Dar
es Salaam leo.
Post a Comment