Jengo la mradi wa viwanda vidogo vidogo lililopo eneo la
Karakana Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Awamu ya kwanza ya jingo
hilo limepangwa kutumia shilingi milioni 190, ambapo inatarajiwa
mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu utakuwa umekamilika kwa asilimia
82.(Picha zote na Christina Mwagala, Ofisi ya Meya wa jiji)
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita mwenye
shati la kijivu akitoa maelekezo kwa maofisa Utumishi wa Halmashauri ya
jiji la Dar es Salaam leo alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya
maendeleo ya jiji karakana ya Mwananyamala jijini hapa.
Mhandisi katika Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam
Swalehe Nyenye akifafanua jambo kwa Mstahiki Meya wa jiji la Dar es
Salaam Isaya Mwita alipofanya ziara ya kutembelea ujenzi wa viwanda
vidogo Karakana ya Mwananyamala.
Mkurugenzi wa kampuni ya Kuja na Kushoka tool Manufucture
Leodard Kushoka akitoa maelezo jinsi namna ambavyo mashine ya
kutengenezea nishati ya mkaa kwa kutumia malighafi inavyofanya kazi
wakati wa ziara waliofanya kwenye kikundi hicho kilichopo Tandika. Wa
kwanza kulia ni Diwani wa Kata ya Segerea Pratrick Asenga.
Mashine inayotumika kutengeneza nishati ya mkaa
Jengo la kikundi cha Upendo Smart kinachofanya shughuli ya kuzalisha nishati ya mkaa kwa kutumia malighafi.
Mwenyekiti wa kikundi cha Mwangaza Vikoba kilichopo Pugu
stesheni Mariam Mzigilwa akisoma risala kwa Mstahiki Meya wa jiji la Dar
es Salaam Isaya Mwita aliyeambatana na wajumbe wa kamati ya fedha ya
jiji leo alipotembelea kikundi hicho, ikiwa ni moja ya ziara ya
kutembelea miradi ya maendeleo ya jiji.
…………………………………………………………………………..
CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI
MSTAHIKI Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo
amefanya ziara ya kutembelea miradi ya Maendeleo ya jiji ambapo
ameridhishwa na vikundi vinavyo tengeneza mkaa kwa kutumia malighafi
ambapo amesema itasaidia kupunguza uchafu uliopo kwenye maeneo
mbalimbali na kuliweka jiji katika hali ya usafi.
Ziara hiyo ambayo imehusisha Kamati ya Fedha ya
Halmashauri ya Jiji, ilitembelea vikundi vya Maendeleo ya ujasiriamali
cha Upendo Smart kilichopo mtaa wa Kilimahewa Kata ya Tandika
kinachojihusisha na uzalishaji wa mkaa mbadala ( mkaa poa).
Aidha mbali na kikundi hicho Meya Mwita pia amejionea
shuguli za uzalishaji wa mkaa unaofanywa na kikundi cha Maendeleo cha
Mwangaza Vikoba kilichopo Pugu stesheni jijini hapa.
Akizungumza na wanakikundi hao, Meya Mwita amesema kuwa
vikundi hivyo vinafanya kazi kubwa kutokana na ubunifu walionao jambo
ambalo litasaidia kuweka jiji kwenye hali ya usafi.
Alifafanua kuwa mbali na kuweka jiji safi pia litapunguza
grama kwa wananchi wanaotumia nishati ya mkaa kutokana na nishati hiyo
kuuzwa kwa bei nafuu ukilinganishwa na ule unaotumika hivi sasa kwakuwa
unagharama kubwa.
” Mmefanya kazi nzuri sana wakina mama ,nimeona juhudi
zenu, lakini nimesikia changamoto kubwa hapa ninamna ya kuwafikia hao
watu waweze kununua nishati hii, niwahakikishie madiwani wenu wapo hapa,
Meya wenu nipo hapa tutaendelea kuwaunga mkono” amesema Meya Mwita.
Amesema” wananchi wanatumia gharama kubwa kununua mkaa
unaochomwa kwa kutumia miti, lakini unapotumia huu ambao unatengenezwa
na vikundi hivi , kwakutumia malighafi , unawezesha kuinua kiuchumi
lakini pia tunatoka kwenye matumizi ya mazoea na kuingia kwenye matumizi
ya kisasa.
Awali ziara hiyo ilianzia kwenye mradi wa ujenzi wa
viwanda vidogo vidogo katika eneo la karakana ya Mwananyamala ambapo
lengo la mradi huo ni kuwahudumia wananchi na wajasiriamali wadogo
wadogo ilikuinua hali za kiuchumi hususani wakina mama na vijana.
Mradi huo unatokana na fedha zilizotengwa na Halmashauri ya
Jiji katika bajeti ya mwaka 2016 /2017 ambapo kwa awamu ya kwanza mradi
huo umepangwa kutumia kiasi cha shilingi milioni 190, hadi kufikia
mwisho wa mwezi huu utakuwa umekamilika kwa asilimia 82.
Hata hivyo Mhandisi wa mradi huo katika Halmashauri ya jiji
la Dar es Salaam Swalehe Nyenye amesema kuwa awamu ya kwanza ya mradi
huo kutajengwa majengo makubwa mawili yenye vyumba vitatu kila moja kwa
ajili ya biashara.
Post a Comment