Waziri wa Ujenzi, Prof. Mbarawa akagua mradi wa barabara za juu TAZARA
…………………………………………………………………
WAZIRI wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa leo amevamia mradi wa
ujenzi wa barabara za juu unaoendelea eneo la Tazara jijini Dar es
Salaam na kuridhishwa na kasi ya ujenzi inayoendelea chini ya Kampuni ya
Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd ya nchini Japan. Akizungumza
katika ziara hiyo alisema lengo ni kuangalia maendeleo ya ujenzi wa
mradi huo ili kuhakikisha unakamilika mapema kama ulivyopangwa.
Prof. Mbarawa alisema
ameridhishwa na maendeleo ya mradi huo ambao mara baada ya kukamilika
utarahisisha shughuli za usafiri kwa wananchi watumiao barabara hizo
mbili za Nyerere na Mandela jijini Dar es Salaam.
Mradi huo wa ujenzi unatarajiwa
kukamilika ifikapo Oktoba 2018 huku ukitarajiwa kugharimu takribani
shilingi bilioni 100, ambapo kati ya fedha hizo shilingi bilioni 93.44
zitatolewa na Japan kupitia Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa (JICA),
na Serikali ya Tanzania itatoa shilingi Bilioni 8.3.
Post a Comment