Wayne Rooney (wa tatu kushoto)
kushoto akiwa na wachezaji wenzake walipokuwa Jijini Dar es Salaam
ambapo timu ya Everton ilicheza na timu ya Gor Mahia katika mchezo wa
kirafiki ulichezwa katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………………………….
Na. Mwandishi Wetu-MAELEZO
Timu ya Soka ya Everton
inayoshiriki ligi kuu nchini Uiungereza imemaliza ziara yake ya siku
mbili nchini Tanzania na kuelezwa kufurahishwa na namna Watanzania
walivyoipokea timu hiyo.
Timu ya Everton iliwasili
Tanzania siku ya Jumatano wiki hii ambapo jana ilicheza mchezo wa
kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia kutoka Kenya.
“Imekuwa ni uzoefu mpya kwangu
kuja hapa (Tanzania) na nina tumaini sasa Makamu wa Rais atakuwa
akiishabikia Everton”, alieleza Wayne Rooney kupitia tovuti ya timu
hiyo.
Pia katika akaunti yake ya
mtandao wa tweeter, Rooney aliwashukuru washabikji wa Tanzania kwa
kuiunga mkono Everton katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya Gor
Mahia kutoka Kenya.
“Great start to the pre-season.
Special thanks to the fans supporting us in Tanzania”, aliandika Rooney
akitoa shukrani za pekee kwa washabiki wa Tanzania.
Kwa upande wa Kocha wa timu hiyo,
Ronald Koeman alielezea kufarahia ziara ya kuja Tanzania na zaidi ni
kutokana na hali ya urafiki iliyooneshwa na washabiki wa soka nchini.
Rooney pia aliungana na wachezaji wengine kama Morgan Schneiderlin, Jonjoe Kenny na Kevin Mirallas
wa timu hiyo walipata fursa ya kujifunza tamaduni za kimsai, kujifunza
kupika chakula cha asili, kutembelea shule yenye wanafunzi wenye
mahutaji maalum na pia kufanya mazoezi na timu ya vijana wenye ulemavu
wa ngozi (Albino United).
Timu ya soka ya Everton ilifanya
ziara nchni Tanzania ambapo ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor
Mahia ya Kenya katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na
kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Rais, Mhe. Samia
Suluhu Hassan ambaye alikuwa Mgeni Rasmi, Marais wastaafu, Ali Hassan
Mwinyi na Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo na wageni mbalimbali kutoka ndani na nche ya nchi.
Post a Comment