Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita |
NA CHRISTINA
MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI
MASHINDANO
ya Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es
Salaam Isaya Mwita ya Ndondo CUP yamemalizika jana ambapo timu ya Sober FC
imeibuka mshindi na kujinyakulia kombe, jenzi pamoja na mbuzi
dhidi ya mahasimu wao Soweto FC.
Katika
mashidano hayo ambayo yalikuwa na mvuto wa aina yake, yalihudhuriwa na wananchi
mbalimbali,viongozi akiwemo mbunge wa
jimbo la Tembeke Abdallah Mtolea, na Madiwani.
Awali mashindano
hayo ambayo yalikuwa na ushidani mkali yalihusisha timu 20 ambapo hadi kufikia
fainali hapo jana timu mbili za Sober FC na Soweto ndio ziliweza kushiriki
hatua hiyo.
Katika
mchezo huo ambao ulifanyika katika viwanja vya Mzimuni ,Kata ya Vijibweni ambapo
Meya Mwita ni Diwani wa kata hiyo, timu ya Sober ilipata ushindi kupitia kwa
mchezaji wao Hassan Gumbo ambae aliipatia timu yake goli la ushindi dakika za lala
salama.
Aidha katika
mashindano hayo, mshindi wa pili ambaye ni Soweto walijinyakulia zawadi ya jezi
pea moja pamoja na mpira huku mshindi wa tatu ambao ni Nondo FC iliibuka na
zawadi ya Mbuzi.
Akikabidhi zawadi
hizo kwa washindi Meya Mwita ambaye ndio mwaandaji wa mashindano hayo, na
Diwani wa kata ya Vijibweni alisema lengo ni kuweka vijana pamoja kwakuwa
michezo ni furaha.
Alifafanua kuwa
licha ya mashinda hayo yaliyomalizika yalihusisha timu kutoka kata moja ya
vijibweni , mashindao yajayo yatahusisha timu kutoka kata mbalimbali ambazo
zitapenda kushiriki.
Katika
mashindano hayo zawadi nyingine zilizotolewa ni pesa tathilimu shilingi 50,000
ambayo ilitolewa kwa mchezaji bora Ibrahimu Kadabla kutoka timu ya Nondo FC.
Hata hivyo
Mbunge wa Temeke Mtolea alisema kuwa
katika mashindano yajayo timu 13 kutoka jimboni
kwake zitashiriki.
Post a Comment