NA CHRISTINA
MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI
HALMASHAURI
ya jiji la Dar es Salaam imepata hati safi kupitia taarifa ya Mkaguzi na
Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini hapa mara baada ya kumalizika kwa baraza la madiwani
la halmashauri ya jiji iliyokuwa na ajenda moja ya kuwasilisha taarifa ya CAG,
Mstahiki Meya Isaya Mwita alisema kuwa hati hiyo imetokana na kuwepo kwa
usimamizi mzuri wa matumuzi ya fedha.
Alifafanua kuwa
kwa kiasi kikubwa tangu alipochaguliwa kushika nafasi hiyo ,jiji la Dar es
Salaam lilisimamia na kupunguza matumizi ya fedha ambayo hayakuwa ya lazima
jambo ambalo limeleta heshima kubwa katika halmashauri hiyo.
Aliongeza
kuwa mbali na hiyo, lakini pia kwa kiasi kikubwa mapato ya jiji yameongezeka
kutokana na kusimamia kikamilifu vyanzo vya mapato vilivyopo ndani ya jiji
hilo.
Alifafanua kuwa
hati hiyo inaleta heshma kubwa ndani ya jiji na kwamba imetoa nafasi kwa
watendaji ndani ya halmashauri kufanya kazi kwa umahiri zaidi ili kuweza kuleta
maendeleo makubwa kwa wananchi.
Alisema taarifa
ya CAG imeeleza wazi kuwa hali ya utekelezaji
ndani ya jiji ni ya kuridhisha kutokana na usimamizi wa kutosha
,kufuatilia mambo na hivyo kuweza kuyafanyia kazi mapendekezo ya ukaguzi wa miaka
ya nyuma yaliyosalia.
“ Baada ya kupata hati hii, sasa niwakati
mwingine jiji kuendelea kufanya kazi za kuwatumikia wananchi ili waweze
kunufaika na rasilimali zao, ukiangalia tumepewa dhamana kubwa ya kuwatumikia
,hivyo kama Meya mwenye jiji sina budi kuwatumikia wananchi kama inavyotakiwa”
alisema Meya Mwita.
Aidha Meya
Mwita alitoa wito kwa halmashauri zilizopo ndani ya jiji la Dar es Salaam
kuwatumikia wananchi ikiwemo kutatua kero zinazo wakabili.
Wakati huo
huo ,Meya Mwita alisema kuwa jiji limetenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya
kununua maeneo ya makaburi kutokana na kuwepo kwa changamoto ya maeneo ya
kuzikia watu.
Alisema kwasasa
hali imekuwa mbaya kwenye maeneo ya jiji na kwamba pesa hizo zitatumika kununua
maeneo ambayo yatatumika kwa ajili ya kuzikia watu wanapopoteza maisha.
“ Jambo hili litaanza kufanyika mwaka huu, kila
halmashauri itapatiwa eneo kwa ajili ya kuzikia watu, yapo maeneo ambayo
tumepanga kuyanunua, ukiangalia jiji letu lina watu wengi sana, kadiri siku
zinavyozidi kwenda ndivyo watu wanavyozidi kuongezeka.
Leo hii
imefikia hatua mtu ana zikwa juu ya mtu mwingine, jambo hili sio zuri, hata
wandishi wa habari leo nikiwaualiza akifa mtu hapa anazikwa wapi, hakuna sasa
utekelezaji wa jambo hili utaanza kufanyika mwaka huu” alisema Meya
Wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmshauri ya jiji la Dar es Salaam wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani lililofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee |
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita
akizungumza na wajumbe wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya jiji, aliyekaa
kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa jiji Waziri Kombo |
Post a Comment