Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimuangalia mhamiaji haramu katika
dirisha dogo la chumba cha mahabusu, Kituo cha Polisi Pangani mkoani
Tanga. Mhamiaji huyo kutoka nchini Somalia alikamatwa wilayani Pangani
katika mwambao wa Bahari ya Hindi. Masauni akiwa mjini Tanga aliwaagiza
Maafisa Uhamiaji na Polisi kuongeza kasi ya kutafuta mizizi ya wahamiaji
haramu mkoani humo. Kulia ni Mkuu wa Kituo Polisi mjini Pangani,
Christina Musyani. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Kituo cha
Polisi cha Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, Christina Musyani wakati
alipokua anamfafanulia masuala ya ulinzi na usalama wilayani humo.
Masauni alikikagua kituo hicho pamoja na nyumba za askari polisi ambazo
zipo katika hali mbaya zaidi kutokana na kutofanyiwa matengenezo kwa
muda mrefu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia) akimsikiliza Mkuu wa Kituo
cha Polisi cha Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, Christina Musyani
alipokuwa anamuonyesha moja ya nyumba ambazo zipo katika hali mbaya
zaidi kutokana na kutofanyiwa matengenezo kwa muda mrefu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitoka kulikagua Gereza la Wilaya ya
Pangani mkoani Tanga. Masauni pia alizungumza na mahabusu wa Gereza hilo
kwa kusikiliza kero zao na kuzitolea maamuzi hapo hapo na baadhi
kuahidi kuzifanyia kazi kwa haraka zaidi. Kwa nyuma ni Mkuu wa Gereza
hilo, Elishinikizo Moshi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimsalimia Mbunge wa Jimbo la Muheza,
Balozi Adadi Rajabu, wakati Naibu Waziri huyo alipowasili wilayani
Muheza mkoani Tanga kwa ajili ya ziara yake ya kikazi. Katikati ni Mkuu
wa Wilaya hiyo, Mhandisi Mwanaasha Tumbo. Kulia ni Mkuu wa Gereza Muheza
ambalo ujenzi wake unatarajiwa kujengwa hivi karibuni baada ya Masauni
kuamuru ujenzi huo uanze mara moja. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya
Muheza, Mhandisi Mwanaasha Tumbo alipokua anatoa taarifa yake ya Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo. Mara baada ya kusomewa taarifa hiyo
na kuona kuna changamoto mbalimbali ikwemo ya kutokuwepo Gereza
wilayani humo, Masauni aliamuru ujenzi wa Gereza hilo uanze mara moja
ikiwa mahitaji yote ya nguvu kazi na mengineyo yapo. Wapili kulia ni
Mbunge wa Jimbo la Muheza, Balozi Adadi Rajabu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Post a Comment