Na: Veronica Kazimoto.
Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania wa awamu ya pili unatarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.
Akizungumza
wakati wa mafunzo ya wadadisi yanayoendelea kufanyika mkoani Dodoma
Meneja wa Shughuli za Kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu
Wilfred Mwingira amesema lengo kuu la utafiti huo ni kufuatilia
viashiria vilivyowekwa kwenye utafiti wa awamu ya kwanza ili kutathmini
na kujua kama kuna athari yoyote iliyotokea.
"Utafiti
huu ni wa kitaifa na utafanyika Tanzania Bara na Zanzibar kwa lengo la
kutathmini na kujua kama kuna athari yoyote iliyojitokeza kwenye
viashiria vilivyowekwa kwenye utafiti wa awamu ya kwanza", amesema
Mwingira.
Nae Mratibu wa
utafiti huo Rainer Kiama amesema kuwa utafiti huu unafanyika ili
kutathmini kama mpango unaleta manufaa yaliyokusudiwa katika ngazi ya
kaya kwa kutumia viashiria kama vile elimu, afya, kazi na matumizi ya
muda, shughuli za kaya zisizo za kilimo, mapato, mikopo, akiba na
uhamishaji fedha.
Viashiria
vingine ni shughuli za kilimo, makazi ya kaya na upatikanaji wa maji,
matumizi na usalama wa chakula katika kaya, maamuzi katika kaya,
ukatili kwa wanawake na matarajio ya vijana, mahusiano ya kaya na jamii
pamoja na mtazamo wa kaya kuhusu Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Utafiti
wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania wa awamu ya pili utahusisha
kaya takribani elfu saba (7,000) ambazo zilihojiwa katika utafiti wa
awamu wa kwanza uliofanyika mwezi Juni, 2015.
Meneja
wa Shughuli za Kitakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Wilfred
Mwingira akizungumza na wadadisi wakati wa mafunzo ya Utafiti wa Mpango
wa Kunusuru Kaya Maskini Tanzania yanayoendelea kufanyika katika ukumbi
wa Chuo cha Mipango mkoani Dodoma.
Wadadisi
wakijifunza kwa vitengo namna ya kutumia vifaa vya kielektroniki -
tablets vitakavyotumika wakati wa Utafiti wa Mpango wa Kunusuru Kaya
Maskini Tanzania unaotarajia kufanyika mwezi Agosti mwaka huu. Mafunzo
ya Wadadisi wa utafiti huo yanaendelea kufanyika katika ukumbi wa Chuo
cha Mipango mkoani Dodoma.

Post a Comment