Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua ripoti ya kwanza ya utawala bora iliyoandaliwa chini ya mpango wa APRM kwa Tanzania, ambapo Tanzania imesifika kuwa kudumisha amani na umoja pia kudumisha Muungano kwa zaidi ya miaka 50.
Rehema
alisema kuwa lengo la APRM ni kuzisaidia nchi za kiafrika, Tanzania
ikiwa mwanachama mmojawapo, kuhakikisha kuwa zinaimarisha utawala bora.
Hii ni kwa kuwashirikisha wananchi wao kubanisha changamoto ili
kuzigeuza kuwa fursa za maendeleo na mambo mazuri ya kuendelezwa kwa
faida ya nchi yenyewe na hata kuwa mfano wa kuigwa na nchi nyingine.
Aidha,
katika ripoti ya mwaka 2012 ilibainisha sifa hizo kwa Tanzania za
kudumisha amani na umoja pia kudumisha Muungano kwa zaidi ya miaka 50,
pamoja na uboreshwaji wa utoaji huduma za kijamii ikiwemo elimu, afya,
maji, usawa wa kijinsia na Teknolojia na habari na mawasiliano (TEHAMA).
Alibainisha
sifa zingine kwa Tanzania “kuwa ni kulinda haki binadamu, matumizi ya
lugha moja ya kiswahili, na hatua za maendeleo ya kiuchumi nchini”
Katibu
huyo alisema kuwa uzinduzi wa ripoti ni utekelezaji wa mojawapo ya
matakwa ya kiutaratibu katika mchakato wa APRM, ikiwa ni kiashiria
kimojawapo cha utekelezaji rasmi ya yale yaliyoandikwa kwenye ripoti
pia kielelezo cha utayari wa Serikali katika kutatua changamoto
zinazowakabili wananchi wake.
Akizitaja
changamoto zinazoikabili Tanzania kutokana na ripoti ya mwaka 2012,
Katibu Mtendaji huyo wa APRM Tanzania alisema kuwa “ katika masuala ya
demokrasia na siasa, hakuna Tume Huru ya Uchaguzi kwa kuwa viongozi wake
ni wateule wa Rais, Taasisi za kuzuia na kupambana na rushwa bado
hazina meno ya kutosha katika kudhibiti rushwa nchini, na kumekuwepo na
migogogro ya ardhi kati ya wazawa na wawekezaji ambapo baadhi ya
wawekezaji wamekuwa wakihodhi ardhi za wazawa bila kutoa fidia kwa
wakati wala kuwapatia maeneo mbadala” .
Naye,
Mkuu wa Kitengo cha Tathimini za Nchi katika Sekretarieti ya APRM na
Mratibu wa Mchakato wa Tananzia Dkt. Rachel Mukamunana alisema kuwa
wanatarajia kuona Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John
Pombe Magufuli ikipatia ufumbuzi changamoto zilizoainishwa katika ripori
ya mwaka 2012.
APRM
Tanzania ilipewa dhamana na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kusimamia majukumu ya nchi katika kuratibu tathimini ya Utawala
bora kwa mujibu wa wa miongozi ya Wakuu wa Nchi za Kiafrika.
Post a Comment