Mkuu wa Wilaya ya Kindoni Mhe
Ally Hapi akishangiliwa na wananchi mara baada ya kuzungumza nao na
kumaliza mgogoro wa muda mrefu wa ardhi katika eneo la Kunduchi Mecco na
mji mpya Kata ya Kunduchi ambao hapo mwanza ilidaiwa na Manispaa ya
Kinondoni kuwa wamevamia kwakuwa eneo hilo lilikuwa limepangwa kwa ajili
ya Machimbo ya Kokoto.
………………………………………………………………………………..
Mkuu wa Wilaya ya Kindoni Mhe Ally Hapi leo ametangaza
msimamo wa serikali ya wilaya ya Kinondoni kuwa wananchi wa Kunduchi
Mecco na mji mpya Kata ya Kunduchi waliokuwa na hofu ya kuondolewa kuwa
hawataondolewa na kwamba badala yake makazi yao yatapimiwa viwanja na
watamilikishwa rasmi.Uamuzi huo umekuja baada ya mvutano wa miaka mingi baina ya manispaa ya Kinondoni na wananchi hao waliovamia eneo hilo ambalo awali lilitengwa kwa ajili ya machimbo ya kokoto. Katika mvutano huo ulioibua kesi mbili zilizoendeshwa kwa muda mrefu na hatimaye manispaa kushinda kesi hizo, uamuzi umefikiwa kuwa Manispaa ya Kinondoni haitawavunjia na kuwaondoa wananchi hao wapatao zaidi ya 3000 waliojenga eneo hilo. Badala yake eneo hilo litapimwa ili kupanga vema mji na kuruhusu maeneo ya huduma za msingi za jamii kama barabara, shule, afya na zahanati kutengewa maeneo.
Akiambatana na Meya wa manispaa
hiyo Benjamin Sitta pamoja na Kaimu Mkurugenzi, Mh. Hapi ameeleza kuwa
serikali ya wilaya itaendelea kumaliza migogoro ya ardhi wilayani humo
na kwamba wananchi waendelee kuiunga mkono na kuipa ushirikiano.
Uamizi huo umepokewa kwa shangwe kubwa na wananchi wa Kunduchi walioamua kumuamuru dereva azime gari la DC HAPI na kulisukuma huku wakina mama wakilifuta vumbi kwa kanga kama ishara ya kufurahia uamuzi huo.
“Leo natangaza rasmi uamuzi wa serikali ya wilaya kuwa
hamtaondolewa hapa.Badala yake mtapimiwa na kumilikishwa kihalali ili
mpewe hati.”Uamizi huo umepokewa kwa shangwe kubwa na wananchi wa Kunduchi walioamua kumuamuru dereva azime gari la DC HAPI na kulisukuma huku wakina mama wakilifuta vumbi kwa kanga kama ishara ya kufurahia uamuzi huo.
Alisema DC Hapi.
Akishukuru kwa niaba ya wananchi wake, diwani wa kata hiyo Mh. URIO ameishukuru serikali kwa uamuzi huo na kwamba wananchi wake wataendelea kuiunga mkono.
Post a Comment