Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akipokewa na Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Ilala, Mhe. Charles Kuyeko alipofanya ziara ya kikazi katika
Manispaa hiyo ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za
watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Wilaya
ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema.
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Sophia Mjema akitoa hotuba ya kumkaribisha
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kuzungumza na watumishi wa
umma katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wakati wa kikao kazi
kilichofanyika katika Manispaa hiyo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Bw, Msongela Palela akiwasilisha
taarifa ya manispaa anayoiongoza kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J.
Kairuki (Mb) alipofanya ziara ya kikazi katika Manispaa hiyo ili kupokea
maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma leo Jijini Dar
es Salaam.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na viongozi na watumishi
wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala alipofanya ziara ya kikazi
katika Manispaa hiyo ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za
watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam.
Sehemu
ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wakimsikiliza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (Hayupo pichani) wakati wa
kikao kazi kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mthibiti
Mkuu Ubora wa Shule – Manispaa ya Ilala, Bi. Juliana Mhonyiwa
akiwasilisha hoja wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha watumishi wa
umma Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J.
Kairuki (Mb) leo Jijini Dar es Salaam.
Serikali
haijafuta mafunzo kwa watumishi wa umma ambapo Taasisi za Serikali
zimeelekezwa kuandaa Mpango wa Mafunzo kwa watumishi kwa njia ya uwazi
na shirikishi ili kuepuka malalamiko kutoka kwa baadhi ya watumishi wa
umma.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na
Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, jijini Dar es
Salaam.
Mhe.
Kairuki amesema mwajiri anapoandaa Mpango wa Mafunzo kwa watumishi wake
ni vyema mpango huo ukawa shirikisha kwa watumishi wote ili kujua
mpangilio wake, ikiwa ni pamoja na kuandaa orodha ya ziada ya watumishi
watakaochukua nafasi za wale waliopangwa kushiriki mafunzo lakini
wakashindwa.
“Napokea
malalamiko mengi sana kuhusiana na upendeleo katika suala la mafunzo,
napenda kuwasisitiza waajiri tuandae Mpango wa Mafunzo ambao ni
shirikishi kwa watumishi wote kuepuka haya, wengine wanapangwa na
hawashiriki mafunzo,” Mhe. Kairuki amesema na kuongeza baadhi ya
watumishi wa umma wanapangwa kushiriki mafunzo na hawaendi kwa sababu
mbalimbali, lakini fursa ya nafasi hizo hawapangiwi wengine ili kuendana
na mpango.
Mhe.
Kairuki ameongeza kuwa Mpango wa Mafunzo shirikishi pamoja na kuondoa
malalamiko, utasaidia pia kutorudisha fedha zilizobaki kwa watumishi wa
umma ambao walipangwa lakini wakashindwa kuhudhuria mafunzo kwa sababu
mbalimbali.
Aidha,
Mhe. Kairuki amesema kwa sababu ya kutoshirikishwa wapo wanaopotosha
kuwa Serikali imefuta Mpango wa Mafunzo. “Napenda kuwaambia kuwa
Serikali haijafuta mafunzo, ili mtumishi wa umma aweze kufanya kazi zake
kwa weledi ni lazima ahudhurie mafunzo,” Mhe. Kairuki amesema na
kusisitiza Serikali inajali mafunzo kwa rasilimaliwatu kwa matokeo bora.
Mhe.
Kairuki yupo katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Dar es salaama
ambapo leo ni siku ya nane akiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
kwa kukutana na watumishi wa umma wa kada zote katika vikao kazi.
Lengo
la kukutana na watumishi wa umma ni kusikiliza malalamiko, ushauri na
changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi ili kuweza
kuzifanyia kazi na kuleta mabadiliko katika Utumishi wa Umma nchini ili
kufikia malengo yaliyopangwa na Serikali.
Post a Comment