Naibu waziri wizara ya Afya,
Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla
akizungumza katika mkutano huo wa wazi kwa wananchi wa Halmashauri ya
Tunduru, Mkoani Ruvuma
Naibu waziri wizara ya Afya,
Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla
akilakiwa na wananchi wa Kijiji cha Mkasale wilayani Tunduru, Mkoani
Ruvuma wakati wa ziara yake hiyo
Naibu waziri wizara ya Afya,
Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla
akimsabahi mmoja wa watoto waliofika na wazazi wake wakati wa kumpokea
katika Kijiji cha Mkasale wilayani Tunduru, Mkoani Ruvuma wakati wa
ziara yake hiyo.
………………………………………………………………
Naibu waziri wizara ya Afya,
Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla
ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tunduru kuhakisha
wanaboresha huduma za Afya katika Wilaya hiyo hasa kituo cha Afya
Mkasale ambacho kimebainika kuwa na huduma mbovu huku pia kikiwa na
uchakavu kwenye majengo yake hali ambayo inaweza kuhatarisha usalama na
afya za watumishi na wagonjwa wanaohudumiwa hapo.
Akiwa katika ziara ya kikazi ya
ukagazi wa utekelezajiwa agizo la uboreshaji wa vituo vya afya katika
kila Kata nchini lilitolewa Desemba 2016, Dk. Kigwangalla akikagua
kituo hicho cha Mkasale , aliweza kujionea mazingira hayo ambapo licha
ya kupewa taarifa alitaka mara moja Uongozi wa Halmashahuri
hiyo kushughulikia suala ndani ya
miezi mitatu ikiwemo Mkandarasi wa Maji kuhakikisha anaingiza mifumo ya
maji ndani ya kituo hicho, pia aliagiza uongozi wa kijiji kushiriki
katika kufanya usafi wa mazingira yanayozunguka kituo hicho cha Mkasale.
Awali akizungumza na wananchi wa
Wilaya ya Tunduru baada ya ziara hiyo ya kukagua vituo vya Afya na
Hospitali ya Wilaya, Dk Kigwangalla amesema Serikali inaendelea na
uboreshaji wa huduma za afya na kuhakikisha kuwa wananchi wanapata
huduma zenye ubora na kwa wakati na lengo la serikali ya awamu ya tano
ni kupunguza kwa asilimia kubwa changamoto zinazoikabili wilaya ikiwa ni
pamoja na kupunguza vifo vya kinamama wajawazito na watoto walio chini
ya umri wa miaka mitano, kukamilisha maboma yote ya vituo vya afya,
zahanati na hospitali ambazo hazijakamilika, na kuhakikisha kuwa vifaa
tiba na dawa zinapatikana za kutosha.
“Hata hivyo nawasihi wananchi
tumuunge mkono Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe
Magufuli kwa vita aliyoianzisha ya kulinda rasilimali za nchi yetu,
kwani taifa limekuwa likiibiwa kwa muda mrefu sana ila umefika muda
kuhakikisha kuwa rasimali za nchi zinatunzwa na kulindwa kwa ajili ya
vizazi vijavyo.” Alieleza Dk. Kigwangalla wakati akiwahutubia wananchi
hao.
Aliendelea kusema kuwa ili
mwananchi aweze kushiriki katika shughuliza uzalishaji ni lazima awe na
afya njema na ili awe na afya njema ni lazima wananchi kwa kushirikiana
na serikali kuboresha vituo vya kutoa huduma za afya na kusogeza huduma
karibu zaidi na wananchi.
“Serikali imeendelea kuboresha
huduma za afya kwa kuhakikisha kuwa dawa zinakuwepo za kutosha katika
hospitali na vituo vya afya na katika mwaka wa fedha 2017/2018 serikali
imetenga bajeti ya kutosha kuhakikisha kuwa vifaa tiba vinakuwepo
katika vituo vya afya na hospitali zote nchini” Alieleza Dk. Kigwangalla
katika mkutano huo.
Samabamba na hayo serikali
inahakikisha kuwa huduma za mama na mtoto zinatolewa bure kwenye
hospitali za umma zote nchi ili kupunguza vifo vya wamama wajawazito na
watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
Dk Kigwangalla aliuagiza uongozi
wa kijiji cha mkasale na mkotamo kutengeza barabara ya kuelekea katika
kituo cha afya mkasale kutoka na barabara hivyo kuwa chafu sana hali
inayoweza kuleta madhara kwa watumiaji hasa kwa wadudu kama nyoka.
“Nakuagiza mwenyekiti wa kijiji
mara baada ya kumaliza kikao hapa upange ratiba na wananchi wako namna
bora ya kuweza kutengeza barabara inayokwenda katika kituo cha afya
mkasale na pia mupange ratiba ya kufanya ausafi katika kituo kwani kazi
ya usafi ni ya wananchi”alisema Dk kigwangalla.
Aidha, katika kuhakikisha
wananchi wanapata huduma zilizo bora uongozi wa wilaya umeagizwa kufanya
kuhakikisha vituo vyote vya afya vilivyopo wilayani Tunduru, vinajenga
vyumba vya upasuaji katika vituo vyote vya afya, kukarabati maabara
zote, na kuhakikisha kunakuwepo na mfumo wa maji safi wenye uhakika
katika vituo vyote vya afya, kufanya matengenezo kwa vifaa vilivopata
hitilafu ili kuboresha huduma.
Post a Comment