Meya wa halmshauri ya Ilala , Charles Kuyeko |
Baadhi ya madiwani wakiwa kwenye kikao. |
NA CHRISTINA
MWAGALA, Dar es Salaam
KUFUATIA
hali ya mvua inayoendelea kunyesha jijini Dar es Salaa , Madiwani wa Halmashauri
ya Manispaa ya Ilala wamesema kuwa ipo haja ya kuweka mipango mikakati ya
kurekebisha miundombinu.
Wakichangia katika
kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Anatoglo leo, madiwani
hao wamesema kwamba hali ya mvua inayoendelea kunyesha imeharibu miundombinu ya
barabara sambamba na kuathiri watu waliokuwa mabonde.
Mbunge wa
jimbo la Ukonga wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Mwita Waitara
amesema kwamba wananchi waliowengi wamejenga nyumba kwenye mikondo ya maji
jambo ambali limesababisha kupoteza makazi yao .
Ameongeza niukweli
usipingia kwamba nyumba zilizojengwa kwenye mikondo ya maji, zilijengwa kimakosa lakini cha kushangaza madiwani waliopo kwenye maeneo yao
wanashindwa kuwaeleza ukweli wananchi madhara ya jambo hilo.
Amesema pamoja na
mapungufu hayo, hivi sasa sio muda wa kuwalaumu wananchi badala yake ipo haya kama
halmashauri kuweka mikakati ya kuwasaidia wananchi sambamba na kurekebisha
mioundombinu hiyo.
“ Nikweli tunatakiwa kukubali kwamba , wananchi walijenga
kwenye maeneo ambayo ni mikondo ya maji, na sisi kama viongozi tukiwa huko
tunashindwa kuwaeleza ukweli wananchi wetu, ila ndio tayari yametokea, sasa
tunapaswa kuweka mpango kwa mwaka mwingine wa mvua kwa ajili ya kurekebisha
miundombinu” amesema Waitara.
Kwaupande wake Diwani wa Kata ya Kipawa wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema, Kenedy Thomas amasema kuwa hali ya miundombinu
ambayo imekuwa kero kwenye maeneo mengi ndani ya halmashauri hiyo inapaswa
kufanyiwa kazi mapema ili kuepuka kero zinazowapata wananchi hivi sasa.
Naye Diwani wa Kata ya Buyuni Twaha Malute wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) ameiomba halmashauri kutenga fungu la zarula ili fedha hizo
ziweze kusaidia kuziba mashimo yaliyopo katika kipindi hiki cha mvua.
Diwani huyo amesema kwamba maeneo mengi yameathirika na mvua
na kwamba hakuna maeneo ya kupita jambo ambalo limenazidi kuwa kero kwa
wananchi katika kipindi hiki kutokana na kujaa maji.
“ Mheshimiwa
Mwenyekiti (Meya wa halmashauri ya Ilala), hali ni mbaya kwenye kata zetu
ambazo tunatoka, njia hazipitiki, niombe halmashauri itenge fungu la zarula turekebishe
hii miundominu ili wananchi njia hizi zipitike kwa urahisi” amefafanua.
Akijibu hoja hizo kwa niaba ya Mkurugenzi wa halmashauri ya
Ilala, Mkuu wa Idara ya miundombinu, ambaye pia ni Mhandisi Mkuu wa
halmashauri, Benjamini Maziku ameeleza kuwa baada ya kumalizika kwa mvua
watafanya tathimini ili kuona maeneo ambayo yameathirika vibaya na mvua na
hivyo kufanya ukarabati.
Ameongeza kwamba kwa sasa hakuna kinachoweza kufanyika
kutokana na hali ya mvua inayoendelea kunyesha ,akawaomba madiwani hao kuwa na
subra ili kupisha kipindi hiki cha mvua kipite na hivyo waanze kufanya
ukaratabati.
“ Naomba jamani tuwe na subra, najua jambo hili ni kero,
lakini kwa sasa hatuwezi kufanya kitu, mikakati iliyopo ni kupisha mvua hii
ambayo inanyesha hivi sasa, ili tufanye ukarabati wa maeneo ambayo yameathirika”
amefafanua Mhandisi Maziku.
Kwaupande wake Meya wa halmashauri hiyo Charles Kuyeko
amesema kwamba maeneo mengi yamekuwa na changamoto ya miundombinu na hivyo
suala la ukaraabati litafanyika ili kuwepo na urahisi wa kupitika katika maeneo
yote.
Post a Comment