Kitaifa, Kimataifa, Siasa, Michezo na Burudani

July 2017

Image result for picha za kassim majaliwa
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewapa siku mbili Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya kumaliza tofauti zao zinazokwamisha utendaji wa Halmashauri hiyo na kuendelea kufanya kazi walizotumwa na wananchi.

Tofauti hizo ambazo zimedumu kwa takriban mwaka mmoja zmesababisha Madiwani hao kushindwa kufanya vikao jambo linalokwamisha shughuli za maendeleo ya wananchi katika Halmashauri hiyo.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Julai 29, 2017) wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela akiwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani Mbeya.

Amesema ikifika Jumatatu (Julai, 31, 2017) Madiwani hao wawe wamemaliza tofauti zao na wawaite wakuu wa Idara na kuwapa taarifa hiyo ili shughuli za maendeleo ziendelee kutekelezwa ndani ya Halmashauri hiyo.

“Baraza la Madiwani limegawanyika mnamgogoro tunataka uishe na mshirikiane na mshikamane katika kufanya shughuli za maendeleo ili wananchi waweze kupata manufaa. Mkiendeleza migongano hatutawavumilia Serikali inauwezo wa tutalivunja baraza.”

Amesema baadhi ya Madiwani hao wanawatetea watumishi waliosimamishwa kazi kwa tuhuma za kuiibia Serikali mabilioni ya fedha jambo ambalo halikubaliki na halivumiliki. “Naombeni mmalize tofauti zenu mara moja kabla sijaondoka.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameiagiza Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mbeya kuhakikisha watumishi wote waliohusika katika kula fedha za umma wanachukuliwa hatua kama alivyopendekeza Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali(CAG).

Pia aliwahasa watumishi wa umma kuhakikisha wanatimiza wajibu na majukumu yao kikamilifu kwa kufanya kazi kwa bidi na kuacha ubabaishaji na kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wawahudumie wananchi ipasavyo.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, JULAI 29, 2017

index
Mkuu wa Wilaya ya Kindoni Mhe Ally Hapi  akishangiliwa na wananchi mara baada ya kuzungumza nao na kumaliza mgogoro wa muda mrefu wa ardhi katika eneo la Kunduchi Mecco na mji mpya Kata ya Kunduchi ambao hapo mwanza ilidaiwa na Manispaa ya Kinondoni kuwa wamevamia kwakuwa eneo hilo lilikuwa limepangwa kwa ajili ya Machimbo ya Kokoto.
………………………………………………………………………………..
Mkuu wa Wilaya ya Kindoni Mhe Ally Hapi leo ametangaza msimamo wa serikali ya wilaya ya Kinondoni  kuwa wananchi wa Kunduchi Mecco na mji mpya Kata ya Kunduchi waliokuwa  na hofu ya kuondolewa kuwa hawataondolewa na kwamba badala yake makazi yao yatapimiwa viwanja na watamilikishwa rasmi.
Uamuzi huo umekuja baada ya mvutano wa miaka mingi baina ya manispaa ya Kinondoni na wananchi hao waliovamia eneo hilo ambalo awali lilitengwa kwa ajili ya machimbo ya kokoto. Katika mvutano huo ulioibua kesi mbili zilizoendeshwa kwa muda mrefu na hatimaye manispaa kushinda kesi hizo, uamuzi umefikiwa kuwa Manispaa ya Kinondoni haitawavunjia na kuwaondoa wananchi hao wapatao zaidi ya 3000 waliojenga eneo hilo. Badala yake eneo hilo litapimwa ili kupanga vema mji na kuruhusu maeneo ya huduma za msingi za jamii kama barabara, shule, afya na zahanati kutengewa maeneo.
Akiambatana na Meya wa manispaa hiyo Benjamin Sitta pamoja na Kaimu Mkurugenzi, Mh. Hapi ameeleza kuwa serikali ya wilaya itaendelea kumaliza migogoro ya ardhi wilayani humo na kwamba wananchi waendelee kuiunga mkono na kuipa ushirikiano.
Uamizi huo umepokewa kwa shangwe kubwa na wananchi wa Kunduchi walioamua kumuamuru dereva azime gari la DC HAPI na kulisukuma huku wakina mama wakilifuta vumbi kwa kanga kama ishara ya kufurahia uamuzi huo.
“Leo natangaza rasmi uamuzi wa serikali ya wilaya kuwa hamtaondolewa hapa.Badala yake mtapimiwa na kumilikishwa kihalali ili mpewe hati.”
Alisema DC Hapi.
Akishukuru kwa niaba ya wananchi wake, diwani wa kata hiyo Mh. URIO ameishukuru serikali kwa uamuzi huo na kwamba wananchi wake wataendelea kuiunga mkono.

pik01
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh.Sophia Mjema akizungumza na madereva wa Bodaboda wilaya ya Ilala baada ya kupokea  maandamano yao leo yaliyokuwa na leongo la  kupongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa Utendaji kazi wake.
Madereva hao walitoa kilio Chao kwa Serikali  kutokana na askari na mgambo kuwakamata mara kwa mara  wakiwa katika shughuli zao za kila siku na kuomba amri ya kukamatwa iondolewa ili waweze kufanya shughuli zao za kutafuta riziki bila usumbufu.
pik1
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh.Sophia Mjema akipokea maandamano ya  madereva wa Bodaboda wilaya ya Ilala leo jijini Dar es salaam kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Ilala Ndugu Edward Mpogolo.
pik2
Baadhi ya wadereva wa Bodaboda wakimshangilia mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema wakati alipokuwa akizungumza nao baada ya kupokea maandamano yao leo jijini Dar es salaam.
pik3
Baadhi ya madereva wa Bodaboda wakiwa katika maandamano hayo.
pik4

PIK1
Balozi wa mchezo wa mpira wa kikapu nchini, Jokate Mwegelo akikabidhi bendera ya Taifa kwa mchezaji Chipukizi, Jesca  Ngaise (katikati)  wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye kituo cha michezo za Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park. Anayeshuhudia zoezi hilo ni Kocha maarufu wa mpira wa kikapu Tanzania, Bahati Mgunda.
KIK3
Balozi wa mchezo wa mpira wa kikapu, Jokate katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji chipukizi wa mpira wa kikapu kwenye viwanja vya JMK Park.
KIK2
Balozi wa mchezo wa mpira wa kikapu, Jokate akisalimiana na wachezaji chipukizi wa mpira wa kikapu kwenye viwanja vya JMK Park.
KIK1
Baba Mzazji wa Jesca, Julius Ngaise akizungumza
………………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu
Balozi wa mchezo wa mpira wa kikapu nchini, Jokate Mwegelo ametoa rai kwa wasichana na wazazi kuwaruhusu watoto wa kike kushiriki katika michezo mbalimbali ili kukuza vipaji na kujiingizia kipato.
Jokate alitoa rai hiyo wakati wa kukabidhi bendera kwa mchezaji chipukizi wa mpira wa kikapu nchini, Jesca Julius Ngaise ambaye anaondoka leo kwenda nchini Afrika Kusini kushiriki katika mafunzo ya juu mchezo huo  yatakayoendeshwa na makocha wa kimataifa wa ligi ya NBA ya Marekani.
Amesema kuwa Jesca ambaye ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Juhudi ya Ukonga, amepata nafasi hiyo baada ya kuchaguliwa na jopo la makocha na kuweka historia ya kuwa msichana wa kwanza wa Tanzania kuhudhuria mafunzo hayo.
“Hii ni faraja kwa Tanzania, makocha wa kimataifa wameona kipaji cha Jesca ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa ya wasichana ya wachezaji wa chini ya miaka 16, ameiwezesha Tanzania kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya Afrika Mashariki nchini Kenya, sasa tunampa bendera na kuiwakilisha nchi katika kozi hiyo, ni sifa kubwa kwake na kwa Taifa,”
“Michezo ni ajira,wachezaji wengi wa mpira wa kikapu wanalipwa vizuri, hii ni fursa kwa Jesca na  wachezaji wasichana, bidii inakuwezesha kufanikiwa, Jesca ni mfano wa kuigwa na sasa anaingia katika vitabu vya kihistoria kwa kuwa msichana wa kwanza kupata mafunzo ya NBA, akifanya vizuri anaweza kwenda Marekani,” alisema Jokate.
Kwa upande wake, Jesca aliwashukuru wote walioshirikiana nao katika mchezo wa mpira wa kikapu na kuahidi kufanya vyema katika kliniki hiyo.
Alisema kuwa hakuamini kupata nafasi hiyo na kuwaomba wasichana wenzake kujishughulisha katika michezo kwani fursa ya kufanikiwa ipo.
“Ni faraja kwangu, wazazi wangu, walimu na wadau wa michezo kwa ujumla, ni heshima kwa Taifa kwani naiwakilisha nchi katika mafunzo hayo, sitawaangusha, nitafanya vizuri na ninaamini makocha wa NBA watavutiwa na kipaji changu na kusonga mbele,” alisema Jesca.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Mwenze Kabinda amempongeza Jesca kwa kupata nafasi hiyo na kuomba kuongeza bidii kwani  hiyo ndiyo njia ya mafanikio.

index
Idara ya Uhamiaji   imesema jukumu la Udhibiti  wa Uingiaji na Utokaji  wa raia  wa kigeni nchini, linatekelezwa kwa mujibu wa Sheria ya Uhamiaji  Sura ya 54 (Rejeo la 2016) na wala  haiwalengi  wafanyakazi  wa  Kampuni ya Madini ya Acacia  peke yake.
 Ni hitajio la kisheria  kwa kila raia wa kigeni  anayeingia na kutoka nchini  kukaguliwa  ili kujiridhisha  iwapo  hakuna  dosari zozote za Uhamiaji, Ulinzi na Usalama.
Sheria ya Uhamiaji inaitaka Idara ya Uhamiaji  kumhoji  mtu yeyote awe raia wa Tanzania au kigeni  bila kujali anafanya  kazi  kwenye Kampuni au Shirika  gani, pale  inapotaka kujiridhisha  juu ya  uhalali  wa ukaazi wake hapa nchini na ikijiridhisha kuwa mtu huyu  hana dosari zozote inamwachia huru kama ilivyofanyika  kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Madini ya Acacia  waliohojiwa  na kuruhusiwa kuendelea na safari yao hivi karibuni.
Idara ya Uhamiaji  inapenda kuuarifu Umma kuwa hakuna sababu zozote  nje ya matakwa ya  Sheria  ya Uhamiaji zinazopelekea  Idara ya Uhamiaji   kuweka kizuizi  cha kuja au kutoka kwa wafanyakazi wa kigeni wa Acacia.
Tunapenda kuujulisha Umma kuwa  ni muhimu  kwa watanzania na raia wa kigeni wanaokusudia kuingia na kutoka nchini kuhakikisha wanafuata  Sheria za Uhamiaji  ili  kutimiza hitajio la kisheria.
Imetolewa na
Ally M. Mtanda
Msemaji wa Idara ya Uhamiaji
29 Julai 2017

1
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipata chakula na manahodha na mabaharia wa meli ya MV Liemba inayofanya safari katika Ziwa Tanganyika.
2
Muonekano wa meli kongwe ya MV. Liemba ikiwa imetia nanga katika bandari ya Kigoma, meli hiyo imeatkiwa kuongeza safari zake kutoka awamu tatu hadi kumi kwa mwezi.
…………………………………………………………………..
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, amewataka manahodha na mabaharia wa meli ya MV. Liemba kufanyakazi kwa ubunifu na uadilifu ili kuiwezesha meli hiyo kujiendesha kibiashara.
Akizungumza na wafanyakazi wa meli hiyo Prof. Mbarawa, ameelezea kuridhishwa na mabadiliko yanayoendelea katika meli hiyo na kuwataka wasibweteke bali waongeze ubunifu.
“Hakikisheni mnatoa huduma bora kwa wateja wenu na kupata faida ili serikali na wadau wengine wawaamini na kutumia huduma yenu”, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Waziri Prof. Mbarawa ameitaka meli hiyo kuongeza safari zake kutoka awamu tatu hadi kumi kwa mwezi ili kuhuisha huduma za usafiri na uchukuzi katika Ziwa Tanganyika.  
Prof. Mbarawa ambaye yuko katika ziara ya ukaguzi wa miundombinu mkoani Kigoma amepata fursa ya kukagua utendaji wa meli ya MV. Liemba, kupata chakula cha pamoja na wafanyakazi wake katika meli hiyo na hatimae kutoa maelekezo kwa manahodha na mabaharia wa meli hiyo kongwe hapa nchini.



NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI

HALMASHAURI ya jiji la Dar es Salaam imepata hati safi kupitia taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2015/2016.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa mara baada ya kumalizika kwa baraza la madiwani la halmashauri ya jiji iliyokuwa na ajenda moja ya kuwasilisha taarifa ya CAG, Mstahiki Meya Isaya Mwita alisema kuwa hati hiyo imetokana na kuwepo kwa usimamizi mzuri wa matumuzi ya fedha.

Alifafanua kuwa kwa kiasi kikubwa tangu alipochaguliwa kushika nafasi hiyo ,jiji la Dar es Salaam lilisimamia na kupunguza matumizi ya fedha ambayo hayakuwa ya lazima jambo ambalo limeleta heshima kubwa katika halmashauri hiyo.

Aliongeza kuwa mbali na hiyo, lakini pia kwa kiasi kikubwa mapato ya jiji yameongezeka kutokana na kusimamia kikamilifu vyanzo vya mapato vilivyopo ndani ya jiji hilo.

Alifafanua kuwa hati hiyo inaleta heshma kubwa ndani ya jiji na kwamba imetoa nafasi kwa watendaji ndani ya halmashauri kufanya kazi kwa umahiri zaidi ili kuweza kuleta maendeleo makubwa kwa wananchi.

Alisema taarifa ya CAG imeeleza wazi kuwa hali ya utekelezaji  ndani ya jiji ni ya kuridhisha kutokana na usimamizi wa kutosha ,kufuatilia mambo na hivyo kuweza kuyafanyia kazi mapendekezo ya ukaguzi wa miaka ya nyuma yaliyosalia.

 Baada ya kupata hati hii, sasa niwakati mwingine jiji kuendelea kufanya kazi za kuwatumikia wananchi ili waweze kunufaika na rasilimali zao, ukiangalia tumepewa dhamana kubwa ya kuwatumikia ,hivyo kama Meya mwenye jiji sina budi kuwatumikia wananchi kama inavyotakiwa” alisema Meya Mwita.

Aidha Meya Mwita alitoa wito kwa halmashauri zilizopo ndani ya jiji la Dar es Salaam kuwatumikia wananchi ikiwemo kutatua kero zinazo wakabili.

Wakati huo huo ,Meya Mwita alisema kuwa jiji limetenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya kununua maeneo ya makaburi kutokana na kuwepo kwa changamoto ya maeneo ya kuzikia watu.
Alisema kwasasa hali imekuwa mbaya kwenye maeneo ya jiji na kwamba pesa hizo zitatumika kununua maeneo ambayo yatatumika kwa ajili ya kuzikia watu wanapopoteza maisha.

 “ Jambo hili litaanza kufanyika mwaka huu, kila halmashauri itapatiwa eneo kwa ajili ya kuzikia watu, yapo maeneo ambayo tumepanga kuyanunua, ukiangalia jiji letu lina watu wengi sana, kadiri siku zinavyozidi kwenda ndivyo watu wanavyozidi kuongezeka.

Leo hii imefikia hatua mtu ana zikwa juu ya mtu mwingine, jambo hili sio zuri, hata wandishi wa habari leo nikiwaualiza akifa mtu hapa anazikwa wapi, hakuna sasa utekelezaji wa jambo hili utaanza kufanyika mwaka huu” alisema Meya
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akiwasikiliza wajumbe wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya jiji waliokuwa wakichangia taarifa iliyowasilishwa kwenye baraza hilo kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG. Katika taarifa hiyo, jiji la Dar es Salaam lilipata hati safi.

Wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmshauri ya jiji la Dar es Salaam wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani lililofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee

Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na wajumbe wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya jiji, aliyekaa kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa jiji Waziri Kombo



Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na wananchi wa eneo la Tegeta kwa Ndevu jijini Dar es salaam, baada ya wananchi hao kusimamisha msafara wake alipokuwa safarini akirejea jijini Dar es salaam kutokea Mkoani Dodoma, Julai 27, 2017.
Sehemu ya wananchi wa eneo la Tegeta kwa Ndevu jijini Dar es salaam, wakimsikiliza Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliposimama kuzungumza nao, alipokuwa safarini akirejea jijini Dar es salaam kutokea Mkoani Dodoma, Julai 27, 2017.
Sehemu ya wananchi wa eneo la Tegeta kwa Ndevu jijini Dar es salaam, wakimshangilia Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliposimama kuzungumza nao, alipokuwa safarini akirejea jijini Dar es salaam kutokea Mkoani Dodoma, Julai 27, 2017. PICHA NA IKULU.

MKRdezign

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget