Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Issaya Mwita na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Benjamin Sitta wakipata maelezo ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) walipotembelea banda la Kampuni hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF) leo. |
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akipata
huduma ya kupima urefu mara baada ya kupima presha alipotembelea banda la
Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) katika Maonesho ya Kimataifa ya
Biashara Dar es Salaam (DITF) leo.
|
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles
Mwijage akiwatambulisha Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe. Issaya
Mwita (kulia) na Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamin Sitta kwa ugeni
kutoka Oman walipotembelea katika Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar
es Salaam (DITF) jana |
NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI
HALMASHAURI zote Nchini zimetakiwa kutumia vyema fedha
zinazotengwa kwa ajili ya kundi la vijana na wanawake katika kuunga mkono
dhamira ya Serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania inakuwa nchi ya
uchumi wa kati na Viwanda.
Hayo
yamebainishwa jijini hapa jana na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya
Mwita alipotembelea Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam
(DITF) ambapo katika ziara hiyo aliambatana na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa
ya Kinondoni Benjamin Sitta.
“Taasisi za
kifedha zinao wajibu mkubwa katika kufikia adhima hii ya Serikali ya Viwanda,
lakini sisi Serikali za mitaa pia , Halmashauri zinazo wajibu mkubwa wa kuhakikisha
kwamba zile asilimia tano za vijana na wanawake zinakuwa sehemu ya kuchochea
ufanikishaji wa dhamira njema ya Serikali hii,” alisema Meya Mwita.
Aidha Meya Mwita ametoa pongezi kwa uongozi wa Tantrade
kutokana na jitihada zao za kuhakikisha wanasaidia ukuaji wa bidhaa za ndani
hasa bidhaa za ngozi ambapo alisisitiza ni vyema wakaendelea kuweka mkazo
katika eneo hilo kabla ya kuangalia maeneo mengine.
Mbali na pongezi
hizo, Meya Mwita aliishauri Tantred kuwa katika kuendeleza dhamira ya maonyesho
ya sabasaba ya Baba wataifa Hayati Julius Nyerere ,ni vema maonyesho hayo
yakafanyika kwa kila mkoa, ili kutoa nafasi kwa wengine kuweza kushiriki
kikamilifu na kujifunza mambo muhimu.
Alisema kuwa
wapo watanzania ambao wangependa kushiriki na kuonyesha bidhaa zao lakini
kutokana na changamoto za hapa na pale wakashindwa kufanikisha na hivyo kukosa
haki yako ya kutoa elimu na kutangaza bidhaa zao.
“ Leo hii
hapa ukiangalia washiriki waliopo kwenye maonyesho haya, ni wahapa, wengine
kutoka nchi nyingine, nakwamba kama wapo wa mikoani sio wote, sasa vipi yule
ambaye yupo Ifakara, Dumila, anabidhaa za kuonyesha lakini kashindwa kushiriki.
Mnaweza kumsaidiaje?,
wakati wa maonyesho haya yalipoanzishwa mwalimu Nyerere alikuwa na dhamira ya
kila mtanzania kutumia nafasi hii kuonyesha bidhaa zake, sasa hili nalo
nashauri mliangalie ili muweze kutoa nafasi kwa kila mtanzania” alisisitiza
Meya Mwita.
wa upande
wake Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta amesema kuwa Maonesho hayo ya
Sabababa yamekuwa na manufaa kwa wafanyabiashara wengi na hata kwa wananchi
kuja kujifunza.
Aliongeza
kuwa pamoja na wananchi kuja kujifunza lakini pia imekuwa ni fursa kwa
wafanyabiashara kutengeneza mahusiano na wafanyabiashara wenzao kutoka nchi
nyingine jambo ambalo katika biashara ni muhimu sana.
Nae, Kaimu
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Edwin
Ratageruka amesema kuwa dhamira yake ni kuhakikisha bidhaa za ndani zinakuwa na
soko la uhakika ndani na nchi ya nchi.
Ameongeza
kuwa kwa kuanzia wamejikita zaidi katika bidhaa za ngozi ikiwa ni njia pia ya
kuwainua wafugaji ambao mazao ya mifugo yao yanatumika katika kutengeneza
bidhaa mbalimbali za ngozi.
“Serikali inatambua umuhimu wa kuthamini
bidhaa za ndani, ndiyo sababu Ofisi ya Waziri Mkuu iliratibu zoezi ambalo jumla
ya vijana 1000 walipatiwa mafunzo ya usindikaji na ushonaji wa ngozi, katika
mafunzo yaliyofanyika Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam tawi la Mwanza,”
alisema Rutageruka.
Rutageruka
ameongeza kuwa katika kuendeleza jitihada hizo Gereza la Karanga (Moshi) na
Kampuni ya Woisso ya Jijini Dar es Salaam zinatarajia kuanzisha viwanda kwa
ajili ya kutengeneza sole ili kuachana na utaratibu wa kuagiza skutoka nje.
Maonesho ya
41 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam yanafanyika huku adhima ya Serikali
ya awamu ya tano ikiwa ni kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya uchumi wa kati
na viwanda
Post a Comment