Na Unique Maringo.
Wakili wa kujitegemea, Jerome Msemwa amejitoa katika kesi namba 213 ya 2017 inayowakabili vigogo wa shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Rais TFF, Jamal Emil Malinzi(57), Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Joas Selestine(46) na Mhasibu wa TFF, Nsiande Isawayo Mwanga(27).
Wakili wa kujitegemea, Jerome Msemwa amejitoa katika kesi namba 213 ya 2017 inayowakabili vigogo wa shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Rais TFF, Jamal Emil Malinzi(57), Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Joas Selestine(46) na Mhasibu wa TFF, Nsiande Isawayo Mwanga(27).
Msemwa ambaye alikuwa akiwatetea
washtakiwa hao, kupitia barua yake ya Julai 5, 2017 aliyoiandika kwa
Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri anaeleza
amejitoa katika kesi hiyo kutokana na kutokupata maelekezo sahihi kutoka
kwa wateja wake hao.
Katika kesi hiyo, inayowakabili
akina Malinzi upelelezi wake bado haujakamilika, itatajwa Julai 17,2017
na washtakiwa wapo rumande kwa sababu miongoni mwa mashtaka
yanayowakabili ya kutakatisha fedha kisheria hayana dhamana .
Washtakiwa hao,
walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Juni 29,2017, wakikabiliwa na
mashtaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha dola za Marekani 375,418.
Katika kesi hiyo, Malinzi anakabiliwa na mashtaka 28 huku wenzake wakikabiliwa na makosa yasiyozidi manne.
Awali, akiwasomea mashtaka
hayo,Wakili wa Serikali Nassoro Katuga alidai katika shtaka la kwanza
kuwa washtakiwa Jamal na Mwesigwa Juni 5,2016 Dar es Salaam kwa nia ya
kudanganya walighushi nyaraka zinazoitwa “Executive Committee
Resolution” za Juni 5,2016 wakionesha kamati tendaji ya TFF imebadili
mtia saini wa akaunti ya benki ya TFF kutoka kwa Edgar Leonard Masoud
kwenda kwa Nsiande Isawafo Mwanga wakati wakijua si kweli.
Katika shtaka la pili, Wakili
Katuga alidai kuwa Septemba Mosi, 2016 katika benki ya Stanbic tawi la
Kinondoni, Mwesigwa aliwasilisha nyaraka ya kughushi.
Katika shtaka la tatu, inadaiwa
kuwa Desemba 17,2013 huko TFF, Jamal Malinzi alighushi risiti namba 308
ya Novemba 6,2013 akionesha ameikopesha TFF dola za Kimarekani 9,300
(sh 19milioni)wakati akijua si kweli.
Katika shtaka la nne, Malinzi
anadaiwa kuwa Desemba 17,2013 katika ofisi hiyo ya TFF, alighushi risiti
namba 322 ya Desemba 17,2013 akionesha ameikopesha TFF dola za Marekani
10,000(sh20milioni) wakati si kweli.
Shtaka la tano, Malinzi anadaiwa
kuwa Desemba 17,2013 katika ofisi ya TFF alighushi risiti namba 323 ya
Desemba 17,2013 akionesha ameikopesha TFF USD 18,000(sh37milioni).
Katuga alidai katika shtaka la
sita kuwa Desemba 17,2013, Malinzi kwenye ofisi hiyo ya TFF alighushi
risiti namba 324 ya Desemba 17,2013 akionesha ameikopesha TFF USD
500(Sh10 milioni).
Katika shtaka la saba, Malinzi
anadaiwa kuwa Desemba 17,2013 katika ofisi ya TFF alighushi risiti namba
325 ya Desemba 17,2013 akionesha ameikopesha TFF USD 1,032(Sh 2milioni)
wakati akijua si kweli.
Katika shtaka la nane
kuwa Machi 26,2014 katika ofisi ya TFF, Malinzi alighushi risiti namba
1956 ya Machi 26,2014 akionesha ameikopesha TFF dola za Kimarekani
40,000(Sh 84milioni) wakati akijua si kweli.
Wakili huyo wa Serikali alidai
katika shtaka la tisa kuwa Machi 13,2014 katika ofisi ya TFF, Malinzi
alighushi risiti namba 1957 ya Machi 13,2014 akionesha ameikopesha TFF
USD 5000(Sh 10milioni).
Aliendelea kudai kuwa katika
shtaka la kumi, kuwa Mei 13,2014 katika ofisi ya TFF, Malinzi alighushi
risiti namba 1624 ya Mei 13,2014 akionesha ameikopesha TFF USD
40,000(sh84milioni).
Katika shtaka la 11, Katuga
alidai kuwa Mei 16,2014 katika ofisi ya TFF, Malinzi alighushi risiti
namba 1634 ya Mei 16, 2014 akionesha ameikopesha TFF USD 10,000(sh20
milioni).
Shtaka la 12, Malinzi anadaiwa
kuwa Julai 11,2014 katika ofisi hiyo ya TFF alighushi risiti namba 1860
ya Julai 11,2014 akionesha ameikopesha TFF USD 15,000(Sh30milioni).
Kwa upande wa shtaka la 13,
Malinzi anadaiwa kuwa Julai 11,2014 katika ofisi hiyo ya TFF alighushi
risiti namba 1861 ya Julai 11,2014 akionesha ameikopesha TFF USD
3,000(Sh 6milioni).
Inadaiwa katika shtaka la 14,
kuwa Julai 15,2014 katika ofisi hiyo ya TFF, Malinzi alighushi risiti
namba 1863 ya Julai 15,2014 akionesha ameikopesha TFF USD 14,000( Sh
28milioni).
Iliendelea kudaiwa katika shtaka
la 15, kuwa Julai 15,2014, Malinzi katika ofisi ya TFF alighushi risiti
namba 1866 ya Julai 15,2014 akionesha ameikopesha TFF USD 4000(Sh 8
milioni).
Katuga alidai katika shtaka la
16, Malinzi anadaiwa kuwa Julai 25,2014 kwenye ofisi ya TFF alighushi
risiti namba 1876 ya Julai 25, 2014 akionesha TFF imeikopesha TFF USD
1,000(Sh 2milioni).
Kwa upande wa shtaka la 17,
wakili huyo wa serikali alidai kuwa Agosti 19,2014 huko TFF, Malinzi
alighushi risiti namba 1890 ya Agosti 19,2014 akionesha ameikopesha TFF
USD 5000(Sh 10 milioni).
Kwenye shtaka la 18, Katuga
alidai kuwa Oktoba 11,2014 kwenye ofisi hizo za TFF, Malinzi alighushi
risiti namba 1568 ya Oktoba 11,2014 akionesha ameikopesha TFF USD 1,200
(2.4milioni) wakati akijua sikweli.
Shtaka la 19, Malinzi anadaiwa
kuwa Agosti 17,2015 kwenye ofisi hiyo ya TFF alikula njama ya kughushi
risiti namba 1511 ya Agosti 17,2015 akionesha ameikopesha TFF
USD 5,000(Sh 10milioni).
Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai akisoma shtaka
la 20, alidai kuwa Julai 22,2015 kwenye ofisi za TFF, Malinzi alighushi
risiti namba 2981 ya Julai 22,2015 akionesha ameikopesha TFF USD
2,000(Sh 4milioni).
Swai akisoma shtaka la 21 alidai
kuwa Mei 9,2016 kwenye ofisi ya TFF, Malinzi alighushi risiti namba 832
ya Mei 9,2016 akionesha ameikopesha TFF USD 7000(Sh14milioni) wakati
akijua si kweli.
Shtaka la 22, Swai alidai Juni
16,2016 katika ofisi ya TFF iliyopo Ilala Dar es Salaam, Malinzi
alighushi risiti namba 931 ya Juni 16,2016 akionesha ameikopesha TFF USD
10,000(Sh20 milioni).
Inadaiwa katika shtaka la 23,
kuwa Malinzi Agosti 2, 2016 katika ofisi ya TFF alighushi risiti namb
947 ya Agosti 2,2016 akionesha ameikopesha TFF USD 1,000(Sh 2milioni).
Akiendelea kusoma hati ya
mashtaka Swai alidai katika shtaka la 24 kuwa Septemba 19,2016 katika
ofisi ya TFF, Malinzi alighushi risiti namba 1029 ya Septemba 19,2016
akionesha ameikopesha TFF USD 1,000(Sh 2milioni).
Swai katika shtaka la 25, anadai
kuwa Septemba 22,2016 katika ofisi ya TFF, Malinzi alikula njama ya
kughushi risiti namba 1071 ya Septemba 22,2016 akionesha ameikopesha TFF
USD 15,000(Sh30milioni).
Kwenye shtaka la 26 ilidaiwa
kuwa kati ya Septemba Mosi na Oktoba 19,2016 washtakiwa Malinzi,
Mwesigwa na Nsiande kwa pamoja na kwa kushirikiana walitakatisha fedha
kiasi cha USD 375,418 huku wakijua fedha hizo ni zao la kughushi.
Katika shtaka la 27, Malinzi na
Mwesigwa wanadaiwa kuwa katika kipindi hicho cha Septemba Mosi na
Oktoba 19,2016 katika benki ya Stanbic tawi la kati la
Kinondoni walijipatia USD 375,418 wakati wakijua fedha hizo zimetokana
na kughushi.
Katika shtaka la
28,Mwanga anadaiw kuwa kati ya Septemba Mosi na Oktoba 19,2016 katika
ofisi ya TFF alimsaidia Malinzi na Mwesigwa kujipatia USD 375,418 kutoka
banki ya Stanbic huku akijua upatikanaji wake umetokana na kughushi.
Post a Comment