WAZIRI Mkuu Kasim Majaliwa ameipongeza timu ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys iliyoshiriki na kutoa upinzani mkubwa kwenye mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika.
Amesema licha ya timu hiyo kumaliza ikiwa na jumla ya pointi 4 sawa na timu iliyoshika nafasi ya pili, ila Vijana hao wameonesha vipaji na uzalendo wa hali ya juu kwa nchi yao.
“Msisitizo wangu kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni kuendelea kuwatunza vijana hao, na kusimamia vilabu vya michezo nchini kuwekeza kwenye soka la vijana ili tujenge timu imara kwa miaka michache ijayo.”
Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua umuhimu wa michezo kwa afya, umoja wa kitaifa na kama fursa ya ajira kwa vijana nchini.
Post a Comment