Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bwana Laurean Bwanakunu (kushoto), akipeana mkono na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa hafla ya kukabidhi jengo la kuhifadhia dawa la Hospitali Maalumu ya Mirembe mjini, Dodoma leo lililokarabatiwa na MSD.
Mkurugenzi
Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bwana Laurean Bwanakunu (kushoto),
akimkabidhi funguo za jengo hilo Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wa hafla hiyo.Kulia ni Ofisa Huduma kwa Wateja wa MSD Mkoa wa Dodoma, Innocent Mugisha.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bwana Laurean Bwanakunu (kushoto), akimuelekeza jambo Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya (wa
pili kulia), wakati wa hafla hiyo. Wengine kutoka kushoto ni Meneja wa
MSD Kanda ya Dodoma, Helman Mng’ong’o na Mkurugenzi wa Hospitali ya
Mirembe, Dkt, Erasmus Mndeme.
Jengo la kuhifadhiwa dawa katika Hospitali ya Mirembe lililokarabatiwa na MSD.
Picha ya pamoja mbele ya jengo hilo lililokarabatiwa na MSD.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Bohari ya
Dawa (MSD) imekabidhi Jengo la kuhifadhia dawa la Hospitali Maalumu ya
Mirembe,Dodoma iliyoifanyia ukarabati wa paa,dari na mfumo wa umeme.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano ya jengo hilomjini Dodma leo asubuhi, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.
Mpoki Ulisubisya amesema inapendeza kwa taasisi za serikali kusaidiana
kuboresha huduma na utendaji pale inapowezekana.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bwana Laurean Bwanakunu amesema mbali na
ukarabati huo,watoa ushirikiano kuandaa makabati ya kuhifadhia dawa
yenye utaalamu unaohitajika.
Ameongeza
kuwa,Hospitali hiyo itaendelea kuhudumiwa kwa upendeleo, ikiwa ni
pamoja na kukopeshwa, kutokana na utofauti wa wagonjwa wanaowahudumia.
Mkurugenzi
wa Hospitali ya Mirembe Erasmus Mndeme ameshukuru kwa msaada huo na
kuomba ushirikiano zaidi na MSD, ikiwa ni pamoja na kupata dawa kwa
maelewano na kumalizia maeneo ya ndani ya kuhifadhia dawa.
Post a Comment