Mwamuzi mtanzania Frank John Komba
ni miongoni mwa waamuzi walioorodheshwa kuchezesha michuano ya Afrika
kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 (U-17 Africa Cup of Nations)
michuano ambayo imepangwa kufanyika Gabon.
Komba yupo kwenye orodha ya
waamuzi wasaidi (Assistant Referees au washika kibendera) na ni mwamuzi
pekee kutoka Tanzania aliyepata fursa hiyo kutoka Tanzania. Komba
anaungana na waamuzi wengine wawili kutoka ukanda wa Afrika Mashariki
Pacifique Ndabihawenimana (mwamuzi wa kati kutoka Burundi na Davies
Ogenche Omweno (mwamuzi wa kati kutoka Kenya).
Hii ni habari njema kwa soka la
Tanzania ambapo wadau wamekuwa wakipaza sauti zao
kutaka wachezaji wa
Tanzania kujituma ili kupata fursa ya kucheza nje lakini pia wamekuwa
wakihoji kwa nini makocha wengi wazawa hawapati nafasi za kufundisha
timu nje ya nchi hali kadhalika kwa waamuzi wa nyumbani wamekuwa
hawapati mechi za kutosha za kimataifa licha ya kuwa na beji za FIFA.
Timu ya taifa ya vijana ya
Tanzania ‘Serengeti Boys’ ni miongoni mwa timu ambazo zitashiriki
michuano hiyo ambayo inatarajia kuanza May 14 mwaka huu.
Shaffihdauda.co.tz inampongeza
Frank John Komba kwa kuteuliwa kuwa miongoni mwa waamuzi watakaochezesha
michuano ya vijana Afrika na kumtakia kila la heri ili afanye vizuri na
kusonga mbele.
Post a Comment