NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Zanzibar, Dk.Abdalla Juma Saadalla “Mabodi” , kwa niaba ya
wafanyakazi na wanachama wote wa CCM amewatumia salamu za rambi rambi
wanafamilia, wa Marehemu Rahma Rashid kilichotokea April 17 mwaka
huu, nyumbani kwake Magomeni Unguja.
Dk. Mabodi alisema Chama
kimepokea kwa masikitiko ,majonzi na huzuni mkubwa taarifa ya kifo cha
aliyekuwa mwanachama wake huyo , ambaye wakati wa uhai wake alijitolea
muhanga kwa maslahi ya CCM.
Alitoa pole kwa familia ya Marehemu na kuongeza kuwa Chama hicho kinaungana na ndugu, marafiki na watu wa karibu wa
na kuongeza kuwa Chama kinatoa
pole kwa familia, ndugu na jamaa wa marehemu katika kipindi hiki kigumu
cha maombolezo ya msiba huo.
Marehemu huyo, ambaye enzi za uhai
wake alikuwa ni mshauri wa Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar
katika masuala ya Sanaa ya utenzi, kazi aliyofanya kwa ufanisi mkubwa.
Alieleza kwamba enzi za uhai wake
Marehemu huyo alikuwa ni miongoni mwa Watunzi mashuhuri wa Tenzi mbali
mbali zikiwemo za kielimu, kijamii na kisiasa ambazo zilimpatia sifa
ndani na nje ya Zanzibar.
“Marehemu Rahma ataendelea
kubaki katika kumbukumbu za Chama chetu kutokana na uhodari wake katika
masuala mbali mbali ya kijamii na kisiasa hasa kwa mambo yaliyokuwa
yakihusu chama chetu.
Wakati wote alikuwa tayari kufanya
kazi za Chama bila ya kujali muda wala maslahi ya binafsi, hivyo na
sisi tuliobaki tukiwa hai kwanza tufuate nyayo zake kwa kuwa
waadilifu na wazalendo kwa Nchi na Chama pia tumuuombee Dua yeye pamoja
na Wazee wetu waliotangulia mbele ya haki uko walipo wapumzike kwa
amani.”, alisisitiza Dk. Mabodi na kuongeza kuwa CCM itaenzi mambo mema
aliyayaacha kwa vitendo.
Wasifu wa Marehemu huyo ambaye
alikuwa ni Mwalimu wa Skuli za msingi hapa Unguja na baadae kuteuliwa
kuwa Mnukuu wa Ikulu Zanzibar na kufanya kazi hapo hadi lustaafu kwake
na amefariki akiwa nab umri wa miaka 69.
Tunaomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Rahma Rashid , Mahala pema peponi . Amin.
Post a Comment