Na Daudi Manongi-MAELEZO.
SERIKALI kupitia Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imechukua hatua mahususi
katika kukabiliana na changamoto zitokanazo na Agenda ya Mabadiliko ya
Umoja wa Ulaya.
Hayo yamebainishwa leo mjini Dodoma leo katika
kikao cha tisa cha mkutano wa Saba wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa
Tanzania na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Suzan Kolimba wakati akijibu hoja mbalimbali za Wabunge
“Umoja wa Ulaya ivi sasa
unatekeleza Agenda ya Mabadiliko ikiwa na lengo la kuongeza ufanisi wa
Sera ya Maendeleo ya Umoja huo,Mabadiliko haya yanahusisha kanuni
mbalimbali za kutoa misaada ya Maendeleo,na mkakati huo umeainisha
maeneo yaliyopewa kipaumbele ikiwemo Masuala ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora,Usawa wa Kijinsia,Vyama vya Kiraia na Serikali za
Mitaa,Rushwa,Sera na Usimamizi wa Kodi na Usimamizi wa Sekta ya
Umma”,Amesema .Kolimba.
Amesema Serikali imechukua hatua
mbalimbali ambazo ni pamoja na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani
na kusimamia matumizi ya fedha za umma ili kuhakikisha tunapunguza
utegemezi kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
Maendeleo.
Pia Serikali inaendelea
kuhamasisha sekta binafsi kushiriki katika utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo kwa kuzingatia Sera ya Ubia baina ya Serikali na
Sekta binafsi ya mwaka 2009 na sheria ya ubia baina ya Serikali na
Sekta binafsi ya mwaka 2010, ambapo mkakati huu unasaidia kuongeza wigo
wa vyanzo za fedha za kugharamia miradi ya maendeleo na kupunguza
utegemezi kwa wahisani.
Hata hivyo Serikali inaendelea
kuwashawishi wawekezaji kutoka nchi mbalimbali kuja kuwekeza zaidi
nchini na zinaenda sambamba na uboreshaji wa mazingira ya kufanyia
biashara nchini na kupunguza gharama za kufanya biashara na uwekezaji
ili kuvutia wawekezaji zaidi kuwekeza nchini.
Katika kuratibu uhamasishaji wa
watanzania waishio ughaibuni Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki imeanzisha Idara maalum ya kuratibu masuala ya Diaspora
ili kushiriki katika Maendeleo ya Nchi ikiwemo kuwekeza nchini.
Post a Comment