Na Daudi Manongi-MAELEZO,DODOMA.
Wizara ya Ardhi,Nyumba na
Maendeleo ya Makazi imesema kuwa Shirika la Nyumba nchini(NHC)
limeweka mkakati wa kuhakikisha nyumba zote zilizo katika hali ya
uchakavu zinafanyiwa ukarabati mkubwa na zile ambazo kiwango cha
uchakavu ni kikubwa zinavunjwa na kuendeleza upya viwanja hivyo.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa
Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula wakati akijibu
hoja mbalimblai za Wabunge leo Mjini Dodoma.
“Shirika la Nyumba la Taifa
limeshafanya uhakiki wa nyumba zake zote na kubaini hali halisi ya kila
nyumba na kuweka mpango wa kuzifanyia ukarabati nyumba hizo kwa
awamu,hata hivyo nyumba ambazo zipo katika hali ya uchakavu idadi yake
sio kubwa ukilinganisha na zilizopo katika hali nzuri na bora
kimatengenezo”,Aliongeza Mabula.
Amebainisha kuwa katika mwaka wa
fedha 2016/17 shirika lilitenga takribani shiingi bilioni 11 kwa ajili
ya kuzifanyia ukarabati nyumba zake ambapo hadi mwezi Machi, 2017 jumla
ya nyumba 2451 zilikuwa zimekwishafanyiwa ukarabati kupitia bajeti hiyo.
Aidha amesema kuwa shirika hilo
linatarajia kumaliza ukarabati wa nyumba zote katika mwaka wa fedha
2017/18 na kusisitiza kuwa matengenezo ya nyumba hizi ni kaiz endelevu
kwa shirika hivyo bajeti ya matengenezo itaendelea kutengwa kila mwaka
ili wapangaji wa nyumba za shirika waendelee kuishi katika nyumba na
mazingira bora.
Post a Comment