Kamati ya Sheria,Katiba na Hadhi za Wachezaji ya TFF
inataraji kutoa maamuzi ya shauri la klabu ya Kagera Sugar inayopinga
kupokwa pointi tatu na kamati ya saa 72 ifikapo mishale ya saa 11 jioni
kwa saa za hapa nyumbani.
Mkurugenzi wa vyama na
uwanachama wa mikoa wa TFF,Eliud Mvela muda huu amezungumza na waandishi
wa Habari ambao wamejitokeza kwenye kikao hicho akiwataka kuwa na subra
au kwenda kuendelea na majukumu yao kisha kurejea muda huo wa saa 11
kwa ajili ya kufahamu kilichojiri ndani ya kmati hiyo.
Mvela alisema kwamba kamati
imeamua kutoa maamuzi kwa muda huo baada ya kuona kuwa kuna mlolongo
mrefu ambao utachukua muda zaidi.
Kikao hicho cha kamati ya Sheria,Katiba na Hadhi za Wachezaji kilianza kulijadili swala hilo kuanzia mishale ya saa nne asubuhi.
Post a Comment