Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsi Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa
Habari (Hawapo pichani) kuhusu uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kuwaajiri madaktari 258
waliotakiwa kwenda kufanya kazi nchini Kenya kulia ni Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo anayeshughulikia Afya Dkt Mpoki Ulisubisya.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsi Wazee na Watoto (anayeshughulikia Afya) Dkt.
Mpoki Ulisubisya akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo
Pichani) kuhusu ugonjwa wa Emofilia ambao umeripotiwa na vyombo vya
habari. kushoto ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsi Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu .
Picha zote na Raymond Mushumbusi Dodoma.
………….
Na Daudi Manongi DODOMA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli ameamua madaktari 258 na wataalamu wa
Afya 11 walioleta maombi na kukidhi vigezo kupitia Wizara ya Afya kwa
ajili ya kwenda kufanya kazi nchini Kenya kuajiriwa na Serikali.
Hayo yamebainishwa leo na Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu
wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari katika Viwanja vya Bunge
Mjini Dodoma.
“Kwa upande wetu sisi ratiba ya
utekelezaji wa ajira hizi za madaktari hao ilikubalika na pande zote iwe
tarehe 6 Aprili 2017 na Madaktari hao wawe tayari kusafiri kwenda
nchini Kenya kati ya tarehe 6-10 Aprili 2017, hadi tarehe ya Taarifa hii
Mahakama nchini Kenya haijaondoa pingamizi lililofunguliwa kuhusu Ajira
za madaktari wa Tanzania nchini Kenya,”Alisisitiza Mhe.Mwalimu.
Amesema kufuatia uamuzi huu majina
ya Madaktari husika na vituo watakavyopangiwa kazi yatatangazwa katika
Tovuti ya Wizara pamoja na wataalamu wengine wa afya 11 walioleta maombi
yao na kukidhi vigezo.
Aidha Serikali ya Tanzania itakuwa
tayari kushughulikia upya ombi la Serikali ya Kenya kupatiwa Madaktari
500, pale ambapo hakutakuwa na vikwazo vya kupeleka madaktari wetu
nchini Kenya.
Mnamo tarehe 18 Machi 2017 Ujumbe
wa Serikali ya Kenya ukiongozwa na Waziri wa Afya Dkt.Cleopa Mailu
uliwasili nchini ambapo ulikutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli kwa madhumuni ya kuomba kuajiri kwa
Mkataba Madaktari wa Tanzania mia tano(500) ili kupunguza uhaba wa
Madaktari nchini Kenya na kukubali ombi hilo.
Aidha Maombi hayo yalipokelewa
ambapo jumla ya maombi 496 yaliwasilishwa na baada ya kufanya uchambuzi
wa maombi hayo ilibainika kuwa Madaktari 258 walikidhi vigezo
vilivyotakiwa kwenda kufanya kazi nchini Kenya,lakini wakati Serikali ya
Tanzania ikiendelea kukamilisha utaratibu wa ajira za Madaktari hao
Madaktari watano wa Kenya waliwasilisha pingamizi mahakamani kuitaka
Serikali ya nchi yao kusitisha kuajiri Madaktari kutoka Tanzania.
Post a Comment