Kamishna Jenerali wa Idara ya
Uhamiaji Dk. Anna Makakala akifafanua jambo kwa waandishi wa habari
(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki wa
uhakiki vibali vya ukaazi ujulikanao kama “E – Verification” mapema
hii leo jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Idara ya
Uhamiaji Dk. Anna Makakala (kulia) akizungumza na maafisa Uhamiaji na
waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki wa
uhakiki vibali vya ukaazi ujulikanao kama “E – Verification” mapema
hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya maafisa Uhamiaji na
waandishi wa habari wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Idara ya
Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mfumo
mpya wa kielektroniki wa uhakiki vibali vya ukaazi ujulikanao kama “E
– Verification” mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Idara ya
Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (kulia) akifuatilia jambo wakati wa uzinduzi
wa mfumo mpya wa kielektroniki wa uhakiki vibali vya ukaazi ujulikanao
kama “E – Verification” mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati
ni Afisa Utawala na Fedha wa Uhamiaji Edward Chegero na kushoto ni Afisa
wa vibali na Pasi wa Uhamiaji Musanga Etimba.
Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo.
Frank Mvungi-Maelezo
Serikali imezindua mfumo wa
Kielektroniki wa Uhakiki wa Vibali vya ukazi “e-verification” hapa
nchini ili kuongeza tija na kudhibiti upotevu wa mapato.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini
Dar es Salaam na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Anna Makakala wakati
wa hafla fupi ya uzinduzi wa mfumo huo.
Akizungumzia mfumo huo Kamishna
Jenerali Makakala amesema utasaidia Makampuni,Taasisi, Mashirika na
watu binafsi kuhakiki vibali vya watumishi wao ili kuona kama ni halali
ama si halali na idara hiyo itakuwa tayari kuwasaidia wale wote
watakaokuwa na matatizo kupata ufumbuzi wa changamoto zao.
“Idara inatoa siku 90 kwa watu
wote kuhakiki vibali vyao vya ukazi ili kama wana matatizo wasaidiwe
kupata ufumbuzi” Amesisitiza Dk. Makakala.
Akizungumzia lengo la mfumo huo
Makalala amesema utasaidia kuimarisha udhibiti wa wageni wanaoishi hapa
nchini na kuzuia mianya ya upotevu wa maduhuli ya Serikali na mfumo huo
ni rahisi na unatoa fursa kwa wageni wote wenye vibali vya ukaazi
kuhakikiki kumbukumbu za vibali vyao ili kujua kama vimetolewa na Idara
hiyo.
Aidha,Idara ya Uhamiaji inawaomba
wadau wa huduma zake kufika wao wenyewe katika Ofisi zao katika ngazi
ya Wilaya, Mikoa na Makao Makuu kwani huduma za Uhamiaji hazina uwakala.
Mfumo huo wa uhakiki wa vibali vya
ukaazi kwa kutumia njia ya kielektroniki “e-verification” unapatikana
kupitia tovuti ya uhamiaji ya www.immigration.go.tz.
Post a Comment