Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mh. Isaya Mwita akizungumza na Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe
wakati alipotembelea katika banda la Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwenye
viwanja vya maonyesho ya biashara vya Mwalimu J.K. Nyerere Barabara ya
Kilwa jijini Dar es salaam.
Mfuko wa LAPF na Jiji la Dar es
salaam wana Mpango kabambe wa kutekeleza ujenzi wa kituo kipya cha
mabasi ya kwenda mikoani jijini Dar es salaam utakaogharimu zaidi ya
shilingi Bilioni 30.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe akitoa
maelezo kwa Meya wa Jiji na Meya wa Kinondoni Mh. Benjamin Sitta
wakati mameya hao walipotembelea katika banda la mfuko huo leo
Meya wa Jiji la Dar
es Salaam, Mh. Isaya Mwita na Meya wa Kinondoni Mh. Benjamin Sitta
wakisaini kitabu cha wageni wakati walipowasili katika banda hilo kulia
ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za
Mitaa LAPF Bw. James Mlowe.
Matukio mbalimbali ya picha
yakiontesha baadhi ya wafanyakazi wa LAPF wakiwahudumia wananchi
waliofika kwenye banda la mfuko wa Pensheni wa LAPF kwenye Maonyesho ya
Sabasaba barabara ya Kilwa leo.
Post a Comment