MWAGALA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia boksi
lililohifadhiwa samaki tayari kwa kusafirisha nje ya nchi wakati
alipotembelea kiwanda cha Kuchakata Samaki cha Musoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania akihutubia wakazi wa Musoma mjini kwenye kiwanja
cha Mukendo ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake mkoani humo. (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
………………………………….
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kamwe Serikali
haitagawa chakula kwa wananchi wavivu ambao hawataki kufanya kazi na
kusubiri chakula kutoka Serikalini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassana ametoa kauli hiyo wakati
akihutubia mamia ya wananchi wa Manispaa ya Musoma katika mkutano wa
hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mukendo mjini Musoma.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu
Hassan amesisitiza kuwa Serikali itapeleka chakula kwa wananchi ambao
mazao yao yaliharibiwa kwa mvua au yalikauka kwa ukame au kwa maafa
mengine na sio kwa wananchi wanaokaa vijiweni mchana kutwa bila kufanya
kazi wakisubiri neema ya chakula kutoka kwa Serikali.
Amewahimiza wananchi kote nchini
kuendelea kufanya kwa bidii ikiwemo shughuli za kilimo na pindi
wanapovuka wajiwekee akiba na waache tabia ya kuuza mazao yote
wanayovuka ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa chakula kwenye familia
zao.
Makamu wa Rais pia amewataka
viongozi wa mkoa wa Mara washirikiane na wananchi katika kuwaelemisha
mbinu bora za kilimo ili waweze kupata mazao mengi ikilinganishwa na
hali ilivyo kwa sasa.
Kuhusu tatizo la uvuvi haramu,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu
Hassan ameziagiza Kamati za Ulinzi na Usalama kufanya misako ya hali na
mali katika kupambana na tatizo hilo ambalo limechangia kupunguza samaki
katika maeneo mbalimbali nchini.
Ametoa mfano kwa mkoa wa Mara kuwa
ulikuwa na viwanda Vinne vya kuchakata samaki lakini kutokana na
shughuli za uvuvi haramu na wa kutumia sumu umepelekea viwanda Vitatu
kukosa malighafi hiyo na kusitisha uzalishaji.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu
Hassan amesema jambo hilo ni baya kwa sababu limeikosesha Serikali
mapato na kusababisha wananchi wakose ajira kutoka kwenye viwanda hivyo
jitihada za makusudi lazima zifanyike katika kukomesha uvuvi haramu
katika maeneo mbalimbali nchini hasa katika Ziwa Victoria.
Aidha, Makamu wa Rais ameeleza
kufurahishwa na kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji wa Musoma ambao
umetekelezwa na Serikali ya Tanzania na Serikali ya Ufaransa na kusema
kuwa mradi huo utaondoa tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama kwa
wananchi wa wilaya ya Musoma.
Amewataka wananchi wa Manispaa ya
Musoma kuulinda na kuutunza mradi huo ili uweze kudumu kwa miaka mingi
kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa Manispaa hiyo.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mara Dakta
Charles Mlingwa amewahimiza wananchi wa mkoa wa Mara kuweka itikadi zao
kando na washirikiane katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
maendeleo mkoani humo.
Makamu wa Rais katika ziara yake
katika wilaya za Butiama na Musoma amekagua shamba la mbegu bora za
muhogo katika eneo la Rwamkoma, Butiama na kuweka jiwe la msingi katika
ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Mutex hadi Buhare yenye
urefu wa kilomita 9.9 katika Manispaa ya Musoma pamoja na kutembelea
kiwanda cha kuchaka samaki cha Musoma.
Post a Comment