Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
amewapandisha vyeo Maafisa watano wa Magereza kuwa Naibu Makamishna na
wengine 24 kuwa Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Magereza kuanzia
tarehe 25 mwezi Mei, 2017.
Waliopandishwa vyeo kuwa Naibu
Kamishna wa Magereza ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Uwesu
H. Ngarama, Boharia Mkuu wa Jeshi la Magereza, Dar es Salaam, Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Gideon M. D. Nkana, Mkuu wa Chuo cha
Taaluma ya Urekebishaji Ukonga, Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Magereza Jeremiah .M.C. Nkondo, Mkuu wa Magereza Mkoa wa
Kagera, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza Tusekile S. Mwaisabila,
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi pamoja na Kamishna Msaidizi Mwandamizi
wa Magereza Augustine S. Mboje ambaye ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es
Salaam.
Waliopandishwa vyeo kuwa
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza ni Kamishna Msaidizi wa
Magereza Mbaraka Sultan Semwanza, Mwalimu wa Hisabati na Kemia shule ya
Sekondari Bwawani inayosimamiwa na Jeshi Magereza, Kamishna Msaidizi wa
Magereza George Togholai Mwambashi, Mkuu wa Kitengo cha Sheria Makao
Makuu ya Magereza Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza Charles
R. Novat, Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo Makao Makuu ya Magereza Dar es
Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza Faustine Martin Kasike Mkufunzi
Mwandamizi Chuo cha Ulinzi wa Taifa (NDC) Kunduchi Dar es Salaam.
Wengine ni Kamishna Msaidizi
wa Magereza Joel Silverster Bukuku, Mdhibiti wa Shirika la Magereza,
Kamishna Msaidizi wa Magereza Deogratius Ndaboine Lwanga, Afisa
Mnadhimu, Magereza Makao Makuu Ukonga, Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi
wa Magereza Boyd Patric Mwambingu, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Pwani,
Kamishna Msaidizi wa Magereza Athuman Ambayuu Kitiku, Mkuu wa Magereza
Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Magereza Hassan Bakari Mkwiche,
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Magereza
Luhende DAVID Makwaia, Mkufunzi Mkuu wa Mafunzo ya Kijeshi na Msaidizi
wa Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira Mbeya, Kamishna Msaidizi wa Magereza
Hamza Rajab Hamza, Afisa Mnadhimu wa Magereza Mkoa wa Tabora na
Kamishna Msaidizi wa Magereza Jeremiah Yoram Katungu, Msaidizi Ofisi ya
Mkuu wa Jeshi la Magereza Makao Makuu Dar es Salaam.
Wengine ni Kamishna Msaidizi
wa Magereza Mzee Ramadhan Nyamka, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro,
Kamishna Msaidizi wa Magereza Afwilile Mwakijungu, Mkuu wa Gereza
Isupilo Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi wa Magereza Ally Abdallah S.
Kaherewa, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi wa Magereza
Salum Omar Hassan, Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Singida, Kamishna
Msaidizi wa Magereza Ismail T. Mlawa, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mtwara,
Kamishna Msaidizi wa Magereza Chacha Bina Jackson, Mdhibiti wa Fedha
Makao Makuu ya Magereza Dar es Salaam na Kamishna Msaidizi wa Magereza
Rajab Nyange Bakari, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Ghasia Magereza
Ukonga Dar es Salaam.
Wengine ni Kamishna Msaidizi
wa Magereza Kijida Paul Mwankingi, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mbeya,
Kamishna Msaidizi wa Magereza Julius Cosmas Ntambala, Msimamizi Mkuu wa
Ujenzi wa Nyumba 320 za Kuishi Askari Gereza la Ukonga, Kamishna
Msaidizi wa Magereza Mussa Musuluzya Kaswaka, Afisa Mkaguzi Makao Makuu
Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza Justine M. Kaziulaya,
Mratibu Msaidizi Baraza la Usalama la Taifa na Kamishna Msaidizi wa
Magereza Bertha Joseph Minde ambaye ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Manyara.
Imetolewa na
Meja Jenerali Projest Rwegasira
Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
6 Juni 2017
Post a Comment