Na Tiganya Vincent-RS-Tabora
Mkuu
wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewataka Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi
na wakuu wa Idara za halmashauri zote za mkoa huo kutoa elimu ya usafi
wa mazingira pamoja na matumizi sahihi ya vyandarua vyenye viuatilifu
vya muda mrefu ili kukabiliana na ugonjwa wa malaria.
Bw.
Mwanri alitoa wito huo jana mjini Tabora wakati akifungua mkutano wa
siku moja kwa viongozi mbalimbali mkoani humo kuhusu mpango endelevu
wa ugawaji wa vyandarua vyenye viuatilifu vya muda mrefu kupitia vituo
vya kutolewa huduma za afya na shule za msingi. Alisema kuwa elimu
sahihi itasaidia wananchi kuacha kutumia vyandarua kwa matumizi mengine
badala ya kujikinga na mbu ili kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa
na malaria .
Mkuu
huyo Mkoa aliongeza wananchi wakifahamu juu ya usafi wa mazingira
utasaidia kuondoa mazalia mbu katika makazi yao. Kwa upande wa Katibu
Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara alitoa wito kwa watalaam kusaidia
mkakati wa kuangamiza kabisa mazalia ya mbu kama sehemu ya kuondoa
ugonjwa wa malaria hapa nchini.
Aidha , Katibu Tawala huyo wa Mkoa
wa Tabora aliiomba jamii kubadirika na kuanza kutumia vyandarua vyenye
viutilifu ili kuokoa maisha ya Mama na mtoto.
Naye Mganga Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Dkt. Gunini Kamba alisema mpango wa kugawa vya ndarua
katika vituo vya kutoa huduma za afya ,shule za msingi na katika ngazi
ya familia unakusudia kupunguza maambuzi ya maralia hapa nchini.
Aliongeza
kuwa vyandarua hivyo vitasaidia kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa
malaria mkoani hapa kutoka asilimia 19.5 ya sasa na kushuka zaidi.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri akifungua Mkutano jana mjini Tabora
wa viongozi mbalimbali kuhusu mpango endelevu wa ugawaji wa vyandarua
vyenye viuatilifu vya muda mrefu kupitia vituo vya kutolea huduma za
afya na shule msingi mkoani humo.
Katibu
Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara akisisitiza umuhimu wa wataalam
kutafuta mbinu ya kuangamiza mazalia ya mbu kama njia ya kukabiliana na
malaria nchini wakati wa mkutano uliofanyika jana mjini Tabora kuhusu
mpango endelevu wa ugawaji wa vyandarua vyenye viuatilifu vya muda mrefu
kupitia vituo vya kutolea huduma za afya na shule msingi mkoani humo. Picha na Tiganya Vincent-RS-Tabora.
Post a Comment