DR. NTUYABALIWE FOUNDATION YAHIMIZA WANAFUNZI KUSOMA VITABU
Mwagala
Wananafunzi wa Shule za
Msingi jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla, wametakiwa kujenga
utamaduni wa kupenda kusoma vitabu vikiwemo vya kiada na ziada, ili
waweze kupanua wigo wa uelewa wa mambo mbalimbali.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi
wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation Mama Jacqueline Mengi, alipozungumza na
wanafunzi, walimu na wajumbe ya Kamati ya Shule ya Msingi Makumbusho,
wakati akizindua maktaba iliyokarabatiwa na mfuko huo.
Amesema upo umuhimu mkubwa kwa wanafunzi kusoma vitabu vya kielimu, historia na pia hadithi.
Awali Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo
Mwl. Bernadicta Lyimo, alitoa shukrani kwa Dr. Ntuyabaliwe Foundation
kwa mchango wake wa vitabu kwa ajili ya maktaba hiyo, na kuomba kupatiwa
mtaalam wa kutunza maktaba, ikiwezekana mwalimu mmoja akasomeshwe
taaluma hiyo.
Naye Afisa Taaluma Fatma Mwiru
akimwakilisha Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni, amewataka waalimu
kuwasaidia wanafunzi kupata vitabu mbalimbali, kwa kuwashirikisha wadau
wa elimu, wachapishaji vitabu pamoja na wahisani.
Aidha Mama Jaqueline Mengi
amesema Dr. Ntuyabaliwe Foundation ilianzishwa mwaka jana ikiwa na lengo
la kuchangia katika sekta ya elimu, ambapo iligundua shule nyingi za
msingi zinakabiliwa na uhaba wa maktaba na vitabu.
Shule ya Msingi Makumbusho
inakuwa ya shule ya pili katika wilaya ya Kinondoni na ya kwanza katika
kata ya Makumbusho, kusaidiwa ujenzi wa maktaba na msaada wa vitabu na
Dr. Ntuyabaliwe Foundation, ikitanguliwa na Shule ya Msingi Hananasifu.
KAWAIDA
Wananafunzi wa Shule za Msingi
jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla, wametakiwa kujenga

Post a Comment