Mchimbaji mdogo wa Madini ya
Almas ambaye pia ni Mshauri Mwelekezi wa SANA Gems Gregory Kibusi,
akiangalia ubora wa Madini ya Alams.
Mshauri Mwelekezi wa SANA Gems
Gregory Kibusi, (kulia), akionesha madini ya Almas . Katikati ni
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ravi Hasmukh. Kulia ni Mkurugenzi Mwenza
Kishan Bhatti.
Madini ya Almas ambayo bado hayajasanifiwa.
Mkurugenzi wa Uthamini wa Madini
ya Almas (TANSORT) kutoka Wizara ya Nishati na Madini Archard Kalugendo
(kulia) akimwonesha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (kushoto) namna
ya kupima ubora wa Madini ya Tanzanite.
Mjiolojia kutoka Kituo cha
Jemolojia Tanzania (TGC) Jumanne Shimba, akiangalia madini kwa kutumia
kifaa maalum cha kinachotumiwa na kituo hicho katika mafunzo.
Mnunuzi wa Madini ya Tanzanite
(kushoto) akiangalia ubora wa Madini ya Tanzanite katika Banda la
Kampuni ya TanzaniteOne. Kulia ni Mwakilishi wa Kampuni ya TanzaniteOne.
Watumishi kutoka Kituo Cha
Jemolojia Tanzania (TGC), wakimsikiliza mgeni aliyembelea banda la kituo
hicho ili kujua shughuli za mafunzo ya usanifu na unga’rishaji wa
madini zinavyofanyika. Mikufu inayoonekana katika picha pamoja na
mapambo mengine imetengenezwa kituo hapo. Kituo hicho kiko chini ya
Wizara ya Nishati na Madini.
Ujenzi wa kisima cha maji
kilichojengwa na Kampuni ya SANA Gems Ltd ikiwa ni sehemu ya kuwezesha
jamii inayozunguka mgodi wa kampuni hiyo kunufaika na uwepo wa mgodi
husika.
………………………..
Na Asteria Muhozya, Arusha
Wachimbaji wadogo wa Madini
walioshiriki Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Madini ya Vito, Arusha
wameiomba Serikali kuendelea kutoa elimu ya uchimbaji bora na uhifadhi
wa mazingira kwa wachimbaji nchini.
Ombi hilo lilitolewa na Mshauri
Mwelekezi wa Kampuni ya SANA Gems, ambaye pia ni mchimbaji mdogo wa
madini ya Almas, Gregory Kibusi.
Kampuni ya SANA Gems inayofanya
shughuli zake za uchimbaji mkoani Shinyanga ndiyo kampuni pekee ya
wachimbaji wadogo iliyokuwa ikionesha madini ya Almas katika Maonesho
hayo.
Kibusi aliongeza kuwa, ushiriki wa
wachimbaji katika maonesho hayo ni fursa kwao ya kukutana na wanunuzi
na kujenga mtandao wa kibiashara hivyo kuiomba serikali kuendelea
kuwahamisha wachimbaji wadogo nchini kushiriki katika maonesho hayo kwa
kuwa, yanawezesha uhakika wa masoko ya madini yao.
“Nikiwa pia kama Katibu Mkuu wa
wachimbaji wadogo Shinyanga, natoa wito kwa wachimbaji nchini kutumia
vyama vyao washiriki maonesho haya ya Arusha kwa kuleta madini yao. Soko
la uhakika lipo,” alisema Kibusi.
Aidha, Kibusi alitumia fursa hiyo
kuwataka wachimbaji nchini kuachana na matumizi ya zebaki na kuwataka
kutumia njia bora zinazoelekezwa na Serikali.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa
Kampuni hiyo Ravi Hasmukh, alisema kuwa, kampuni hiyo imeshiriki
Maonesho hayo ili kuweza kujenga mtandao wa kibiashara ikiwemo pia kutoa
fursa kwa Watanzania kujifunza namna Madini ya Almas yanavyochimbwa na
mahali yanapopatikana.
Aidha, ameitaka Serikali ifikishe
umeme katika eneo hilo na maeneo mengine mbapo shughuli za uchimbaji
mdogo zipofanyika ili kuwezesha kuharakisha maendeleo ikiwemo kuwezesha
shughuli za kiuchumi na kupanua wigo wa ajira.
Akizungumzia namna kampuni hiyo
inavyosaidia eneo linalozunguka mgodi wake alisema kuwa, kampuni hiyo
imetengeneza kisima cha maji kwa ajili ya kijiji cha Hukiro pamoja na
kuboresha baadhi ya miundombinu katika zahanati iliyo jirani na mgodi
wa kampuni hiyo
Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Vito
Arusha yalifunguliwa rasmi tarehe 3 Mei na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt.
Joel Bendera na kufungwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
Post a Comment