Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati), akimsikiliza Katibu Mkuu
(Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (Kulia), mara baada ya kumaliza
kuwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha 2017/2018. Kushoto
ni Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Eng. Deusdedit
Kakoko.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipongezana na Watendaji wa Wizara
hiyo mara baada ya kumaliza kuwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka
wa Fedha 2017/2018.
Watendaji wa Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano wakipongezana mara baada ya Bunge la Bajeti
kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha 2017/2018.
Mtendaji Mkuu Wa Shirika la Reli
Nchini (TRL), akizungumza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George
Masaju mara baada ya Bunge la Bajeti kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa
mwaka wa Fedha 2017/2018.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Post a Comment